Fonolojia ya kimachame na kiswahili:
Kabila la wachaga ni kabila ambalo linapatikana mkoani
Kilimanjaro. Kabila hili hutumia lugha ya kichaga ambayo huwaunganisha wachaga
wa maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo kama vile Machame, Kibosho, Rombo,
Marangu, Siha, Kishumundu na Oldi Moshi. Kutokana na tofauti za kijiografia
lugha ya hii imegawanyika katika vilugha (lahaja) ambapo vilugha hivyo hutajwa
kimaeneo kama ilivyo hapo juu. Hivyo, katika ufafanuzi huu tutajikita katika
kichaga cha MACHAME lakini tutatumia neno la jumla yaani kichaga. Kama ilivyo
katika lugha ya kiswahili na lugha nyinginezo, lugha ya kichaga inaweza
kuchanganuliwa katika vipengele mbalimbali kupitia tawi la isimu nyanjani kama
ifuatavyo:
1 Fonolojia
ya lugha ya kichaga.
Kwa mujibu wa Roger (1994), fonolojia ni tawi la isimu
linaloshughulikia uamilifu, tabia na mpangilio wa sauti katika lugha. Kwa maana
hiyo, fonolojia ni tawi la isimu linalojihusisha na uchunguzi, ufafanuzi na
uchanganuzi wa sauti katika lugha mahususi kuanzia inapotamkwa, namna
inavyotamkwa sehemu zinazohusika katika utamkaji na namna inavyosafiri na
kupokelewa na msikilizaji. Dhana za msingi katika fonolojia ni fonimu na
alofoni. Katika kipengele hiki tutaangazia fonimu za lugha ya kichaga kama
ifuatavyo:
Fonimu |
Sauti |
Mfano |
a |
/a/ |
/amba/ - sema |
b |
/b/ |
/bara/ - pasua |
c |
/tꭍ/ |
/tꭍamԑtꭍa/ - pole |
d |
/d/ |
/dԑŋga/ - laani |
e |
/ԑ / |
/ԑla/ - peta |
f |
/f / |
/fɪꭍa/ - vunja |
i |
/ ɪ/ |
/ɪrɪꭍa/ -
subiri |
k |
/k/ |
/kaꭍa/ -
zamani |
ky |
/kj/ |
/kjaasɔ/ -
methali |
l |
/l/ |
/ʊlaalʊ/ -
sasa |
Ly |
/ly/ |
Lya - kula |
n |
/n/ |
/naa/ - kunywa |
ng' |
/ŋ/ |
/ŋana/ - kua |
ny |
/ɳ/ |
/ɳaɳ/ - mboga
za majani |
m |
/m/ |
/mmɪ/ - mume |
o |
/ɔ/ |
/ɔra/ - onyesha |
p |
/p/ |
/para/ - pasua |
r |
/r/ |
/raa/ - vaa |
r |
/ɣ/ |
/ɣa/ - acha |
s |
/s/ |
/sɔka/ -
teremka |
sh |
/ꭍ/ |
/ꭍɪa/ - njia |
t |
/t/ |
/tԑɣԑβa/ -
omba |
u |
/ʊ/ |
/ʊkwa/ -
wehuka |
v |
/β/ |
/βandʊ/ - watu |
w |
/w/ |
/waa/ - uwa |
y |
/j/ |
/jԑwԑ/ - wewe |
Katika uchambuzi huu, fonimu nyingi za lugha ya
kichaga zinaendana na fonimu za lugha ya kiswahili lakini kwa baadhi ya fonimu
kama vile /r/ na /v/ hutumika kulingana na muktadha wa matumizi. Katika baadhi
ya maneno fonimu /r/ hutumika kurejelea sauti /r/ lakini katika maneno mengine
huwakilisha sauti /ɣ/. Vile vile fonimu /v/ huwakilisha sauti /v/ na pengine
hurejelea sauti /ß/.
2. Aina za maneno.
Aina za maneno ni mkusanyiko wa maneno yenye sifa zinazofanana
ambayo huwekwa katika makundi mahususi. Mathalani maneno yanayotaja vitendo
huwekwa katika kundi moja la vitenzi na maneno yanayotaja majina huwekwa katika
kundi la nomino. Lugha ya kichaga ina aina mbalimbali za maneno lakini katika
kipengele hiki tutaangazia aina nne ambazo ni Nomino, vitenzi, vivumishi pamoja
na vibainishi kwa kutaja na kuonesha tafsiri zake katika Kiswahili.
A. NOMINO.
Hili ni kundi la maneno ambalo hutaja majina ya watu,
vitu, hali na mahali.
NA. |
NOMINO ZA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
|
NA. |
NOMINO ZA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
1 |
Ifua |
Mfupa |
|
21 |
Mbaka |
Paka |
2 |
Ifururu |
Bundi |
|
22 |
Mburu |
Mbuzi |
3 |
Ifuve |
Nyani |
|
23 |
Mmi |
Mume |
4 |
Ikite |
Mbwa |
|
24 |
Mmiku |
Babu |
5 |
Ikokoi |
Panya |
|
25 |
Mmbishwa |
Shetani |
6 |
Ikoru |
Konokono |
|
26 |
Mmbwa |
Mvua |
7 |
Ikunga |
Samaki |
|
27 |
Mwana |
Mtoto |
8 |
Iriso |
Jicho |
|
28 |
Mwi |
Jua |
9 |
Iruu |
Ndizi |
|
29 |
Saa |
Nuru |
10 |
Iruva |
Mungu |
|
30 |
Samu |
Damu |
11 |
Kana |
Mdomo |
|
31 |
Sava |
Funza |
12 |
Kasa |
Pori |
|
32 |
Soko |
Maharage |
13 |
Kiafuye |
Kinyonga |
|
33 |
Soori |
Nguo |
14 |
Kilwa |
Chura |
|
34 |
Shaa |
Njaa |
15 |
Kiri |
Kiti |
|
35 |
Shau |
Dume |
16 |
Kisaa |
Makalio |
|
36 |
Shoka |
Nyoka |
17 |
Kisangu |
Uso |
|
37 |
Shoonga |
Chakula |
18 |
Kishomba |
Kiswahili |
|
38 |
Shuki |
Nyuki |
19 |
Kisi |
Kiuno |
|
39 |
Ukari |
Ugali |
20 |
Kiriya |
Nyundo |
|
40 |
Uluko |
Kijiko |
41 |
Mai |
Mama |
|
46 |
Upata |
Kata |
42 |
Maruu |
Ndizi |
|
47 |
Uraato |
Upepo |
43 |
Urende |
Mguu |
|
48 |
Mangi |
Mfalme |
44 |
Usavi |
Uchawi |
|
49 |
Nlosha |
Mwalimu |
45 |
Uvayo |
Unyayo |
|
50 |
Nsongoru |
Kiongozi |
B. VITENZI
Vitenzi ni kundi lenye aina za maneno ambayo hueleza
jambo lililofanyika, ambalo hufanyika, linalofanyika au litakalofanyika. Kwa
ujumla hutaja matendo mbalimbali ambayo hufanywa kwa namna na nyakati tofauti.
Miongoni mwa viitenzi katika lugha ya kichaga ni kama vifuatavyo:
NA. |
VITENZI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
|
NA. |
VITENZI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
1 |
Afua |
Tambaa |
|
11 |
Bara |
Pasua |
2 |
Akua |
Kopa |
|
12 |
Basha |
Chonga |
3 |
Amba |
Sema/ pakaa |
|
13 |
Dosha |
Toboa |
4 |
Ana |
Lia/ shukuru |
|
14 |
Ekyena |
Hesabu |
5 |
Anga |
Ingia |
|
15 |
Ekyera |
Egesha |
6 |
Angata |
Futa |
|
16 |
Ela |
Peta |
7 |
Ara |
Laza |
|
17 |
Faka |
Kunya |
8 |
Arannya |
Sikiliza |
|
18 |
Fina |
Cheza |
9 |
Ata |
Washa/ ingiza |
|
19 |
Fira |
Kaba |
10 |
Ava |
Gawanya |
|
20 |
Fisha |
Vunja |
NA. |
VITENZI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
|
NA. |
VITENZI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
21 |
Fumbuta |
Ongeza |
|
36 |
Kumba |
Uza |
22 |
Fwaaya |
Samehe |
|
37 |
Kummbwa |
Kumbuka |
23 |
Fweesa |
Pooza |
|
38 |
Kura |
Kwangua |
24 |
Illwa |
Ng'oa |
|
39 |
Lallwa |
Bandua |
25 |
Imuya |
Pumzika |
|
40 |
Lema |
Kataa |
26 |
Ira |
Pita |
|
41 |
Lelemba |
Bembeleza |
27 |
Irisha |
Subiri |
|
42 |
Lemba |
Danganya |
28 |
Isa |
Chunga |
|
43 |
Leta |
Mimina |
29 |
Ishura |
Jaza |
|
44 |
Lola |
Angalia |
30 |
Iva |
Iba |
|
45 |
Maa |
Maliza |
31 |
Kaba |
Piga |
|
46 |
Na |
Kunywa |
32 |
Kama |
Kamua |
|
47 |
Onga |
Nyonya |
33 |
Kira |
Ponya |
|
48 |
Raa |
Vaa |
34 |
Komba |
Lamba |
|
49 |
Tarama |
Saidia |
35 |
Kora |
Pika |
|
50 |
Ura |
Nunua |
Katika orodha hiyo, baadhi ya vitenzi vina maana zaidi
ya moja mfano, "amba" ina maana ya kupakaa kama kupaka rangi lakini
kwa upande mwingine ina maana ya sema kama kusema jambo. Hivyo muktadha wa
matumizi na toni ndio hutambulisha maana iliyokusudiwa.
C. VIVUMISHI
Rubanza (2003:72-75) anasema kuwa kivumishi ni kipashio
kitoacho habari zaidi kuhusu nomino. Kwa maana hiyo, tunaweza kusema kuwa hili
ni kundi la maneno ambayo hufanya kazi ya kuifanya nomino au kiwakilishi
kivume. Hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino au viwakilishi. Vivumishi
vinavyopatikana katika lugha ya kichaga ni hivi vifuatavyo katika jedwali.
NA. |
VIVUMISHI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
|
NA. |
VIVUMISHI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
1 |
Shaa |
Nyeupe |
|
11 |
Shisha |
Nzuri |
2 |
Shaangu |
Nyepesi |
|
12 |
Shikasha |
Mbaya |
3 |
Shaasha |
Ndefu |
|
13 |
Siise |
Embamba |
4 |
Shiroo |
Nzito |
|
14 |
Shiwongye |
Nene |
5 |
Shuu |
Nyeusi |
|
15 |
Iilye |
Safi |
6 |
Shuumu |
Ngumu |
|
16 |
Ifani |
Chafu |
7 |
Rola |
Tamu |
|
17 |
Shidodoru |
Nyekundu |
8 |
Shifii |
Fupi |
|
18 |
Shikuu |
Chakavu |
9 |
Shiniini |
Kubwa |
|
19 |
Shiiya |
Mpya |
10 |
Shinnywa |
Ndogo |
|
20 |
Shinana |
Laini |
D. VIBAINISHI
Kibainishi ni neno ambalo hutumika pamoja na nomino nalo
kwa kiasi fulani huweza kuonyesha ukomo wa maana ya nomino (Richards na
Schmidt, 2002: 152). Vibainishi ni maneno ambayo hufanya kazi ya kutoa taarifa
zaidi zinazoihusu nomino. Ni maneno yenye dhima ya kisarufi yanayotumika
kuonyesha aina ya kirejelewa ambayo nomino hiyo inayo kama vile idadi, nafsi,
uhusika, ngeli, dhamira na jinsi. Vipo vibainishi mbalimbali ambavyo
vinapatikana katika lugha ya kichaga. Navyo ni:
NA. |
VIBAINISHI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
|
NA. |
VIBAINISHI VYA KICHAGA |
TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI |
1 |
Umwi |
Mmoja |
|
11 |
Ungi |
Mwingine |
2 |
Vavii |
Wawili |
|
12 |
Engi |
Pengine |
3 |
Vararu |
Watatu |
|
13 |
Toose |
Zote |
4 |
Vaana |
Wanne |
|
14 |
Tawo |
Zao |
5 |
Yeu |
Huyu |
|
15 |
Mfumbutu |
Mwingi |
6 |
Eva |
Hawa |
|
16 |
Shiingi |
Nyingi |
7 |
Valya |
Wale |
|
17 |
Fiingi |
Vingi |
8 |
Kulya |
Kule |
|
18 |
-eeru |
- etu |
9 |
Eyo |
Hiyo |
|
19 |
-afo |
-ako |
10 |
Yewo |
Hao |
|
20 |
-any |
-enu |
3. Ngeli za nomino.
Ngeli ni neno lililotokana na lugha ya kihaya
"ingeli" lenye maana ya "kundi" au "aina". TUKI
(1990) wanaeleza kuwa, ngeli ni kundi moja la majina yaliyo na upatanisho wa
kisarufi unaofanana na viambishi vya umoja na wingi vinavyofanana. Kwa maana
hiyo, ngeli inaweza kufasiliwa kuwa ni namna ya kuweka majina katika makundi
yanayofanana au kuwiana kwa kuzingatia sifa za majina hayo. Uainishaji wa ngeli
za nomino hufanyika kwa kuzingatia vigezo mbalimbali kama vile kigezo cha
kutumia viambishi vya upatanisho wa kisarufi na kigezo cha umoja na wingi.
Aidha katika uchanganuzi ufuatao wa ngeli za nomino za kichaga tutatumia kigezo
cha upatanisho wa kisarufi pamoja na umoja na wingi.
NA. |
NGELI |
UFAFANUZI |
MIFANO |
1 |
A - VA |
Hii ni ngeli inayojumuisha majina ya watu na nafasi
zao. Majina kama vile Mwana (mtoto), Mwiisi (mchungaji), Mai (mama), Mfuru(daktari),
Nde (baba), Nlosha (mwalimu) Mmiku (mzee), Nkyeku (bibi), Nsee (mtoto wa
kiume) na Nka (mke) |
·
Mwana akelya Vana vakelya ·
Mmiku ansha Vamiku vansha |
2 |
I - TI |
Kundi hili huwa na majina ya wanyama, ndege na
wadudu kama vile Ng'umbe (ng'ombe), mburu (mbuzi), nguve (nguruwe), fiko
(fuko), nguku (kuku), saafu (siafu), sisiri (sisimizi), ngoru (mwewe), shoka (nyoka), nre (nzige), mbaamba (kumbikumbi)
|
·
Mburu ikeana Mburu tikeana ·
Nguku ikeshishwa. Nguku tikeshishwa |
3 |
KI - FI |
Ngeli hii huwakilisha majina ambayo mwanzoni huwa na
herufi KI. Majina hayo huweza kuwa ya vitu, wanyama na wadudu. Majina hayo ni kama vile kiri (kiti),
kyaandu (kisu), kibeni (kizibo), kimwi (kijinga), kilwa (chura), kifi
(nyigu), kite (mbwa). |
·
Kiri kikesongosywa Firi Fikesongosywa ·
Kilwa Kikekillya Filwa Fikekillya |
4 |
LYI - A |
Kundi hili huhusisha majina yote yanayoanza na kiambishi
[i-] katika umoja na kiambishi [ma-] katika wingi mfano, iriso (jicho) -
mariso (macho), iyoo(jino) - mayoo (meno),
isosoro(mjusi) - masosoro (mijusi), Isembo(mjinga) - masembo(wajinga) Irimbi(mshenzi)- marimbi(washenzi) |
·
Iyoo elyi lyikevava Mayoo yaa akevava ·
Iriso lyilolye fo Mariso alolye
fo ·
Isembo lyikeiya Masembo akeiya |
5 |
U |
Hili ni kundi lenye majina ambayo huanza na
kiambishi [u-] na ambayo hayana wingi. Mfano uraato(upepo), u |
·
|
|
A /KU |
Hii ni ngeli inayoonesha mahali. Ni sawa na ngeli ya
"PA/MU/KU" katika kiswahili. Katika lugha hii kuna viambishi viwili
tu. |
·
Ando alya aleera ·
Kundo kulya Kutanywe ·
Kulya kukeremwa ·
Yoo kuketirika |
5 |
|
|
|
4. Mfumo wa uhesabishaji
Kama ilivyo katika lugha ya kiswahili na lugha
nyingine, lugha ya kichaga ina namna ya uhesabuji wa namba kwa idadi zote
zilizopo. Hii inadhihirika kama ifuatavyo.
i)Namba kuanzia moja hadi kumi.
o
Kimwi
- moja
o
Fivii
- mbili
o
Firaru
- tatu
o
Fiina
- nne
o
Firanu
- tano
o
Firindaru
- sita
o
Mfungare
- saba
o
Nyanya
- nane
o
Kyenda
- tisa
o
Ikumi
- kumi.
i) Makumi, kuanzia kumi hadi mia moja kwa kigawe cha
kumi kwa mumi.
o
Ikimi
- kumi
o
Makumi
avii - ishirini
o
Makumi
araru - thelathini
o
Makumi
aana - arobaini
o
Makumi
aranu - hamsini
o
Makumi
arindaru - sitini
o
Makumi
mfungare - sabini
o
Makumi
nyanya - themanini
o
Makumi
kyeenda - tisini
o
Iyana
- mia moja
iii) Mamia, kuanzia mia moja hadi elfu moja kwa kigawe
cha mia kwa mia.
o
Iyana
- mia moja
o
Mayana
avii - mia mbili
o
Mayana
araru - mia tatu
o
Mayana
aana - mia nne
o
Mayana
aranu - mia tano
o
Mayana
arindaru - mia sita
o
Mayana
mfungare - mia saba
o
Mayana
nyanya - mia nane
o
Mayana
kyenda - mia tisa
o
Kyiku
- elfu moja.
Mfumo huu wa uhesabishaji unazingatia mfumo wa hesabu
wa mamoja, makumi, mamia, maelfu na kuendelea. Baada ya kutaja namba kubwa
ndipo namba nyingine hufuata kwa kadiri ya udogo wake kama ilivyo katika lugha
ya kiswahili. Mfano, "Kyiku kimwi na mayana avii na ikumi" yaani elfu moja na mia mbili na kumi. Pia
baada ya kila kundi moja la namba (1-9) uhesabuji hufanywa kwa kurudia au
kuongeza namba za awali. Mfano baada ya kufika kumi, ili kuendelea unarudia
tena kuitaja kumi na kuongeza namba za mwanzoni yaani moja hadi tisa ndipo
ufike katika kundi lingine. " ikumi + kimwi = ikumi na kimwi, mayana avii
+ kimwi = mayana avii na kimwi".
5. Mfumo wa uitaji majina kwa watu.
Mfumo wa uitaji majina hutofautiana baina ya jamii na
jamii. Katika kabila la wachaga watu hupewa majina kama sehemu ya
kuwatambulisha kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo ni pamoja na hali,
ukoo, dini pamoja na idadi ya wazaliwa. Hivyo, tutaanza kufafanua kipekngele
kimoja baada ya kingine kama ifuatavyo:
a) Hali
Hii inahusisha hali inayokuwapo wakati mtoto anazaliwa
hivyo kupelekea kuitwa jina linaloendana na hali hiyo. Majina hayo ni pamoja
na:-
·
Ifura
- Furaha (hutokana na hali ya furaha)
·
Nsia
- Tumaini (hutokana na hali ya kupata tumaini baada ya masumbuko)
·
Ndetyefyose
- Baba ameyasikia yote ( hutokana na hali ya kupata tumaini)
·
Alewarywa
- Aliyepokelewa (Ni jina la mtoto aliyesubiriwa kwa shauku kubwa)
·
Widimi
- Uwezo (ni jina linaoonyesha hali ya kuwa na uwezo wa kupata watoto)
b) Idadi ya wazaliwa
Kila mzaliwa katika familia huwa na jina lake la
jumla. Majina haya huwataja babu na bibi wa pande zote na hulenga kuonyesha
heshima pamoja na kuendeleza undugu na mshikamano wa familia na ukoo kwa
ujumla. Aidha jina la mtoto wa kwanza ni moja kwa kila mtoto wa kwanza kwa
kuzingatia jinsia. Majina haya si mahususi yaani siyo ya mtu binafsi ( jina la
shule au ubatizo) bali ni ya nyumbani. Majina hayo ni kama yafuatayo.
·
Mkuu/
Meku/ Nkuu- Jina la mzaliwa wa kwanza wa
kiume. Humtaja babu kwa upande wa baba kwa maana hiyo "nkuu/ Meku" ni
vifupisho vya neno "mmiku" yaani babu.
·
Kyekuwe
- Hili ni jina la mzaliwa wa kwanza wa kike. Sifa zake ni sawa na
zinazorejelewa na zile za mzaliwa wa kwanza wa kiume lakini humrejelea bibi. Ni
jina lililotokana na neno "nkyeku" likiwa na maana ya bibi na
kiambishi "we" humaanisha "yake" hivyo ni sawa na kusema
bibi yake. Hii ni kwa upande wa baba.
·
Ndeyanka
- Ni jina la mzaliwa wa pili wa kiume. Jina hili humtaja baba mzaa mama (baba
mkwe). Katika jina hili neno "nde" humaanisha baba halikadhalika neno
"nka" humaanisha mke na "ya" ni kiunganishi. Kwa maana hiyo
ni sawa na kusema baba wa mke yaani baba mkwe.
·
Mayeanka/
Manka - Hili ni jina la mzaliwa wa pili wa kike. Ni jina ambalo humtaja mama
mkwe au bibi kwa upande wa mama ambapo "ma/maye" ni mama,
"a/ya" ni viunganishi na "nka" ni mke. Hiyo, ni sawa na
kusema mama wa mke yaani mama mkwe.
· Mamii - Ni jina la mzaliwa wa tatu wa kike. Humtaja mama mzaa baba yaani babu kwa upande wa baba. Limetokana na maneno "ma" ikiwa ni kifupisho cha "maye a" "yaani mama wa" pamoja na neno "mii" likiwa na maana ya "mume". Hivyo hutaja mama wa mume ambapo ni sawa na mama mzaa baba.
·
Ndammi
- Hili ni jina la mtoto wa kiume linalomrejelea babu kwa upande wa baba. Hili
huweza kuwa kwa mzaliwa wa tatu na kuendelea japo ni sawa na jina la mzaliwa wa
kwanza.
Katika orodha ya wazawa wa kiume kuanzia wa tatu na
kuendelea jina la " Nkuu" huendelea kwa kurejelea babu kwa upande wa
baba. Hutajwa kwa hesabu kuanzia wa pili hadi wa mwisho kulingana na idadi
iliyopo yaani, "nkuu wa kavii (wa pili)", "wa kararu (wa tatu)" na kuendelea.
Mathalani kwa wazawa wa kike "Mamii" pia huendelea kwa kumtaja bibi
kwa upande wa baba kama ilivyo kwa upande wa wazawa wa kiume.
c). Dini ( Kikristo)
Baada ya ujio wa wamishenari katika eneo la uchagani
watu waliopokea mafundisho walibatizwa na kuwa wafuasi wa dini ya kikristo. Hii
ilipelekea kuiingiza dini katika mfumo wa lugha ili kuweza kuendeleza shughuli
za kidini. Vitabu vya dini hususani Biblia vilitafsiriwa kwa lugha ya kichaga
yakiwemo majina ya waandishi na watu waliotajwa katika vitabu hivyo. Hivyo watu
hupewa majina mara baada ya kubatizwa. Majina hayo ni pamoja na haya yafuatayo:
·
Anandumi
- Mshukuru Bwana
·
Anande
- Mshukuru Baba (Mungu)
·
Eliakunda
- Mungu amependa
·
Elianshisauwa
- Mungu amenichagua
·
Elianshiwinya
- Mungu amenishindia
·
Rumishaeli
- Mtukuze Mungu
·
Aranyandumi
- Msikilize Bwana
·
Ndemfoo
- Baba (Mungu) ni mpole
·
Shikusiriyaeli
- Ninamtumaini Mungu.
·
Simboyande
- Kipawa cha baba (Mungu)
d) Koo (ukoo)
Ukoo ni muunganiko wa familia zenye asili moja. Ni
vizazi mbalimbali vilivyotokana na familia moja. Majina ya ukoo hutambulisha
watu kuwa wametokea katika familia fulani. Aidha kila mtoto anayezaliwa katika
familia ya ukoo fulani hupewa jina la mwisho la ukoo wa familia hiyo. Hata
mwanamke anapoolewa pia huwa na jina la ukoo wa familia ambayo ameolewa.
Miongoni mwa majina hayo ni haya yafuatayo:
·
Swai
·
Sawe
·
Kimaro
·
Lema
·
Mushi
·
Nkya
·
Urassa
·
Usiri
·
Ulomi
·
Mmbasha
6. Lugha na jinsia
Katika lugha ya kichaga, lugha hutumiwa kulingana na
jisia katika baadhi ya shughuli mbalimbali za kila siku. Kuna maneno ambayo
huwakilisha jinsia moja tu na mengine huwakilisha jinsia zote. Kwa msingi huo
lugha hujipambanua katika vipengele vifuatavyo:
a) Salamu
Kuna salamu ambazo hulenga jinsia ya kike tu na zile
ambazo hulenga jinsia ya kiume. Salamu kwa upande wa jinsia ya kike huwa na
neno "ma" kumaanisha mama, "kye" kumaanisha binti au
msichana na "nkwe" kwa maana ya mtu yeyote wa kike. Mfano,
·
Neantwa
ma - salamu ya asubuhi kwa mama
·
Nesindiswa
kye - salamu ya mchana kwa msichana au binti
·
Kwalollya
nkwe - salamu ya jioni kwa wanawake wote
Kwa upande wa jinsia ya kiume, salamu huwa ni ile ile
lakini huwa na maneno ambayo hurejelea jinsia ya kiume mwishoni. Neno
"mbe" huwakilisha mtu ambaye ni baba, "mae" huwakilisha
kijana wa kiume na "nsee" huwakilisha kijana mdogo. Aidha wakati
mwingine "mbe" hurejelea wanaume wote. Mfano,
·
Neantwa
mbe - Salamu ya asubuhi kwa mtu mzima (baba).
·
Nesindiswa
mae - Salamu ya mchana kwa kijana.
·
Kwalollya
nsee - Salamu ya jioni kwa mtoto. ( pia hutolewa baada ya kazi)
b) Majina
Utoaji wa majina huzingatia jinsia. Kuna majina ambayo
ni ya wanawake na mengine ambayo ni ya wanaume tu. Majina hayo ni pamoja na
yale ya idadi ya wazaliwa. Mfano:
Wanawake.
·
Manka
·
Kyekuwe
·
Mankya
·
Mansabu
·
Mamii
Wanaume
·
Ndeyanka
·
Babuu
·
Meku
·
Nkuu
·
Ndeanshau
Kwa ujumla, Lugha ya kichaga ni lugha inayojitosheleza
kwa kuweza kukidhi haja ya mawasiliano katika shughuli mbali mbali. Aidha
hutumika katika maeneo ya nyumbani, katika vikao vya vijiji pamoja na kanisani.
Lugha hii pia ina maandiko mbalimbali ikiwemo vitabu vilivyotafsiriwa kutoka
lugha nyingine. Miongoni mwake ni kitabu cha Agano jipya, Biblia pamoja na
vitabu vya nyimbo za ibada. Kwa maana hiyo, ina uwezo wa kuchanganuliwa kupitia
taaluma ya isimu kama ilivyo katika lugha ya kiswahili.
Lass, R. (1984). Phonology: An introduction to Basic
Concepts. Cambridge: Cambridge Textbooks in Linguistics.
Richards, J. C & Schmidt, R. (2002). Longman
Dictionary of Language Teaching and Applied Linguistics: 3rd Edition,
London: Pearson Education Limited.
Rubanza, Y.I (2003). Sarufi: Mtazamo wa Kimuundo.
Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar
es Salaam: TUKI.