Saturday, July 6, 2019

HISTORIA YA KABILA LA WACHAGA

HISTORIA YA KABILA LA WACHAGA,


WACHAGA,  Ni moja ya makabila yanapatikana katika nchi/Taifa la TANZANIA, Ni kabila la watu wenye  asili ya KIBANTU Lakini pia Ni mchanyiko wa DAMU hasa ya (KIKUSHI) wanaoishi kaskazini mwa TANZANIA chini ya mlima KILIMANJARO...

WACHAGA.... Ni kabila la tatu apa  nchini kuwa na idadi ya watu wengi  kwa Takwimu za mwaka 2003 kwa kuwa na idadi ya watu 2,000,000/= 

    NENO UCHAGA lina  historia ndefu sana, inaelezwa kwamba misafara ya wafanya biashara iliyokuwa ikiongozwa na waarabu walipokuwa wakipita maeneo ya VUNJO Waliwaona wenyeji wakiwa wamejenga VIBANDA vya kulinda mazao yao  yasiharibiwe na wanyama wakawa wanawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi VICHAKANI wageni wafanyabiashara na wamisionari walipokuwa wanakuja KILIMANJARO walielekezwa na waongoza misafara kwamba wanaenda nchi ya UCHAKANI wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani hatimae wageni wakashindwa kulitamka neno hill vizuri na kulitamka UCHAGANI nalo likabaki kuwa jina la sehemu hii malo hutumika adi sasa.

SHUGHULI kubwa ya WACHAGA Ni BIASHARA,KILIMO NA KAZI ZA OFISINI.
  
WACHAGA... Ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima KILIMANJARO mashariki hadi magharibi 

JIOGRAFIA ya mashariki Rombo,Tarakea  unawapata watu wa Mwika,kilema,Marangu,Mamba na Kirua ambayo inajulikana na watu wengi kamaVunjo......

Jiografia ya magharibi wanaoishi wamachame unapata watu wa Oldmoshi,wa-kibosho,wa-uru,wa-Siha na wa-machame 

Imeandaliwa na sirGeorge Boaz sway ndeyanka

Msaada wa .........
Mtandao
Maktaba
Masimulizi ya kale onlinetechersway.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

061058168