Friday, May 29, 2020

SALAMU ZA KIMACHAME;, KAMUSI YA MANENO YA KICHAGA NA MAAANA ZAKE.


kwalolya na mashora mbuya yakwa kwifyenda? Kukundee ikuloshaa iidikira kwa kimashamii? embu eta mariso daa-te

Maneno ya kichaga (kimachame) na salamu za kichaga

salamu za kimachame

NB:

mmi=mume

Nka=mke

Mbee=baba

Mma=mama

Kyaa= rika wa kike

Mwaa=rika wa kiume

Mfamau= dada yako

Munamau=kaka yako

Muneru=mdogo wetu wa kiume/kike

Nkyeku= bibi

Mmiku=babu

Mbuya=rafiki

Ngama=asubuhi

Nantwa-mbe-umeamkaje /kwa wanaume

Nantwa-ma-umeamkaje/wanawake AU

kwaantwa fo inda- kisha unaongezea neno la mtu huyo au kiwakilishi chake mfano(Nantwa-mbe,mma,kyaa,mmiku nk)

Nsanyii=mchana

Neisindiswa-mbe-umeshindaje /baba

Neisindiswa-ma-umeshindaje/ kwa mwanamke AU

Kwasindafo-inda- kisha unaongezea neno la mtu huyo au kiwakilishi chake mfano(Nantwa-mbe,mma,kyaa,mmiku nk)

Nkwaany=Jioni

Salamu za wakati huu hufanana na salamu za mchana tu unaweza zitumia hadi muda wa 11:00 jioni

Nkyo-o=usiku

Huwa ni kuagana kwa ajili ya kulala kwa kusema....

Lwarwakisha-mbe,mae,kyaa

lwarwakisha=Tulazwe salama

SALAMU FUPI MPYA ZA VIJANA

Mbony=Mambo

Nyinda=vipi

Shivya=Nambie

Maneno ya kimachame na maana yake

Msoro/Msero- mtoto wa kiume

Mfu- mafuriko

aika/Eka-asante

Tarambwa-panua

kulasaree-fo -usijali

Fiterewo-maombi

Lya-mboo-apa

Lolaa-ona

Wakwe-wake(vandu wakwe=watu wake)

ai-yo- yupo

Kwankooya- ukimpata

Vaanga-ita

Muni-mwenyewe

urere-umbeya

Ifura-kufurahi/furaha

Mmi-Mume

Mka-mke

Ndami-baba yake mumeo

Mammiy- mama yake mume

Mkyeku/mcheku/ msheku - bibi

Mmiku/ meku- babu

Boo/ kyeni/kyan-nyumbani

Mkunde- mpendwa

Itondo-mjinga

isembo-mpumbavu

Mukha/ mringa- maji

Memba/maemba-mahindi

Soko/ maraki-maharage

Mshele-mchele

Mburu-mbuzi

Nguku-kuku

Ngumbe-ngombe

Yanri-Kondoo

Kite-mbwa

Mbaka-Paka

Ifuru-ru-Bundi

Ingala-kaa

kinyany-Mamba

Iketi-Mtu ambaye ajaoa

Shonga-Chakula

Kyandu-kisu

Upanga/ubanga-Panga

Ibengele-kisu/panga butu

Nungu-chungu

Muruwa/malela-maziwa

Mnswa-uji

Iseka-mwanaume ambaye hajatairiwa

Mwi-Jua

Mbwaa-Mvua

kwafo-kwako

ikusaro-mawazo

uvangiso-ubarikio

lumwaani-tumshukuru

Iruwa-Mungu

Mbishwa-Shetani

Kifuu-kaburi

vifuu-makaburi

Safari-kyaro

Inyinyi-Mwizi

mashora-kazi

kindo- kitu

inu-leo

Ngama-asubuhi

Nrima-moyo

Floose-vyote

Mang'aa-malaya

ikokoi-Panya

Isosoro-Mjusi

Ngurana-mtoto wa mbuzi

Ilemba-kudanganya

Udede-Ukweli

Ngama-asubuhi

Nsanyiny-mchana

Nkwany-jioni

Nkyoo-usiku

Mashora-kazi

Kwalolya-pole na kazi

Itumwa-kunyonga

Intiratira-kumshikashika

Isangya-kuosha

Masara-nguo

Ulaalu-sasa

Numa-nyuma

Indouwa-kumjibu

Ekyo kukundye- hicho unachokipenda

Ando amwi-mahali pamoja

Lumiso-kushoto

oko lusha/ndumi- mkono wa kulia

Kufii-karibu

Indo-fo -hivyo hapana

Kitatauri-kipepeo

Tira-shika

wuya-rudi

Kwakooya-ukikuta

Indi-hivi

Maako-mikono

mini-vidole

Lweende-tuende

Iimuya-kupumzika

Kwaasha-mbali

Kwasha-pole kwa safari

Naasa-basi

Soori-nguo

kyighami-nguo iliyochakaa

Karibuni sana kwa atakayehitaji maana/Tafsiri ya neno fulani nitamwambia kwa kichaga inaitwaje.

Shukrani kwa mdogo wangu Celina Boaz kwa ushirikiano wake kwangu.

Natumaini umefurahi sana kwa kufahamu baadhi ya maneno ya kichaga na maana yake.

Kwa maoni ushauri nitafute kwa:

MAWASILIANO

Tell+255 621 058168=Whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com

Google: Mwalimu george boaz

facebook: sirGeorge Boaz

HAI

KILIMANJARO


No comments:

Post a Comment

061058168