AFYA NA USAFI KWA KIJANA

SURA  YA KWANZA

AFYA NA USAFI KWA KIJANA 

(zaburi 119:9)

Afya: Ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili , kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na madhari au magonjwa yoyote. Ili mwanadamu aweze kuwa  na afya nzuri anahitaji kula mlo kamili, kufanya mazoezi na usafi wa mwili.

Hivyo basi kama mwili huitaji hayo ili kuwa na afya njema . Roho nayo huhitaji chakula cha kiroho, chakula cha kiroho ni neno  la Bwana . Unapofanyia mwili wako mazoezi na usafi kumbuka pia kufanyia na moyo wako.

Kijana unapaswa kuwa safi na nadhifu kila mda, kwani kwa kutokuwa safi huweza kukufanya kubaguliwa na hata kuwa na marafiki wachache na pengine kukosa kabisa .Baadhi ya vijana huweka suala la usafi na kujali afya zao pembeni na kuzani akisha  kuoa/kuolewa ndio anapaswa kula vizuri na kuvaa pia. Mwonekano wa kijana ndio huweza kumpa hadhi au kumshusha hadhi.

Mambo ya kuzingatia katika usafi 

Usipende kurudia rudia  nguo  bila ya kuzifua

Usivae wigi moja wiki au mwezi

Oga mtumishi

Mashuka na nguo nyingine  (soksi ,boxer na nguo za ndani) fua mara kwa mara

Kula mlo kamili

Usibanie hela hadi unashindwa kujijali

Vaa vizuri (nguo za heshima )

Pima afya mara kwa mara mtumishi

Usipende kuendana na fashion

Lugha yako iwe nzuri (zungumza kwa staha)

Nyoa au suka mtindo mzuri rafiki

Lisha roho yak0 chakula

Na mengine mengi kuwa  msafi wa rohoni na mwilini ni jambo jema. Kumbuka bila ya afya nzuri na unadhifu wa mwili usingeweza kusoma kitabu hiki.

Ujana ni kipindi kilichopo kati ya utoto na uzee katika maisha ya binadamu, Kipindi cha ujana huanzia miaka 18 mpaka 45 kwa tafsiri ya sheria ya Tanzania. Maisha ya binadamu huwa na vipindi vitatu utoto,ujana na uzee. Vipindi vyote hivi mwanadamu hufurahia sana  kipindi cha ujana na huona ndicho kizuri. Mambo mengi na mazuri hufanyika katika kipindi cha ujana mfano kuoa/kuolewa, kupata watoto na mengine mengi.(mhubiri 11:9)

Tunajua kuwa hakuna jambo linalowezekana kwa mwanadamu kufanya akiwa dhaifu kimwili, Pia kuna mambo hatuwezi kufanya tukiwa wazee au watoto hivyo ujana ni kipindi cha peke yake. Tunaweza sema ujana ni leo na uzee ni kesho hivyo kesho(uzee) nzuri hutegemea leo(ujana) Mungu alitumia watumishi wengi wakiwa na nguvu yaani wakiwa vijana mfano Abeli,meshack, shedrack, daudi, Yusufu, Sulemani na wengineo wengi maandiko yanatuasa kuutumia ujana wetu vizuri kwani ndicho kipindi pekee cha maisha ya binadamu chenye nguvu. (1yohana 2:14B, methali 20:29A) 

Bwana mungu anahitaji sisi vijana tumkumbuke kwani tuna nguvu si ya mwilini tu pia kiroho, Kumkumbuka bwana katika ujana ni kwa namna na hali tofauti mfano kumwimbia, kufundisha neno lake, kufanya huduma kama uinjilisti, kufanya kazi za mikono kanisani na kumtolea bwana. Ujana huwa ni kipindi hatari sana sio kiroho tu ata kimwili shetani amezua mambo mengi ambayo hufanya vijana kushawishika na kutoufurahia ujana wao. Uasherati,uzinzi,kunywa pombe,uvutaji sigara,kwenda kumbi za kileo,umalaya na uongo, vyote hivi hutoka kwa shetani na huaribu kabisa vijana (1yohana 2:15) Maandiko pia yanatuasa ili ujana wetu uwe kielelezo chema yatupasa kuwa safi (2timotheo 2:22)     

Kwenye maombolezo 3:27 Maandiko yanatufundisha kuwa ujana ndicho kipindi cha kuchukua nira yetu, Zipo nira nyingi sana ambazo ni nzuri na nyinginezo ni mbaya maishani mwa kijana. Unapotazama (mathayo 11:29-30) Yesu anatuasa tuchukue nira yake kwani ni laini na mzigo wake ni mwepesi. Lakini pia anatuasa tusichukue nira mbaya katika (2wakoritho 6:14). Tumkumbuke mungu siku za ujana wetu kwa  kuwa karibu na mungu na kufanya mambo mema kama niliyotaja hapo juu na mengine yanayofaa mbele za mungu kama kusaidia wahitaji (mhubiri 12:1) kwani kwa kufanya hivyo mungu hukumbuka maagano yetu ya ujanani (ezekiele 16:60)  Tunaposhirikisha mungu katika maisha yetu ya ujana hutufanya kuufurahia ujana wetu (mhubiri 11:9).

Tunapoenda kinyume na maandiko na maagizo ya mungu hufanya ujana wetu kudharauliwa na wenzetu,watoto na hata wazee. (1timotheo 4:12) 

MAMBO YA KUFANYA KAMA KIJANA KABLA UJAFIKISHA MIAKA 25

Weka akiba

Nunua kiwanja vifaa vya ndani kama kitanda godoro vyombo na thamani.

Anzisha vyanzo vya uchumi

Kuwa karibu na mungu

Tafuta mchumba

Umejiwekea mambo gani ya kufanya kabla ya kufikia umri huu embu taja mambo matano.

Maandiko yanasemaje (zaburi 119:9) Ili kijana aweze kuwa na mwenendo safi anapaswa pia (zaburi 119:10).

Dhambi ni uasi kama maandiko yasemayo neno uasi ni kwenda kinyume na taratibu/sheria/maagizo/kanuni/maelekezo au maonyo kwa lugha nyepesi. Kwa kujua yapi upaswi kwenda kinyume nayo kama kijana katika mienendo yako utaweza kuwa na maisha ya utukufu na kielelezo chema kwa jamii mfano kijana mwenzetu (mwanzo 39:26-28) aliweza kukimbia zinaa kwa kujua atavunja amri za MUNGU (1wakoritho6:18). Pia maandiko yanatuasa ili tuweze kuwa safi kiroho na kimwili kama vijana yatupasa kuacha baadhi ya mambo (2Timotheo 4:12). kwani kwa kufanya hivyo ujana wako hautadharauliwa bali utakuwa ni kielelezo chema kwa wakutazamao (1Timotheo 4:12).


No comments:

Post a Comment

061058168