Tuesday, July 28, 2020

UKWELI KUHUSU WANAWAKE WA KIMACHAME KUUWA WAUME ZAO.


KWA NINI WANAUME WA KICHAGA HUFA MAPEMA KULIKO WAKE ZAO...
Jambo hili la wanaume wa kichaga hususani machame kuanza kufariki kabla ya wake zao limezua mjadala sana, Wengine wamediriki ata kutooa Uchagani (mmachame) kwa kuhofia kutatishwa maisha yao, Eti kwamba wanawake wa kichaga huuwa wanaume zao pale tu wanapotajirika. 
Huku Wengine wamehusisha jambo hili na imani za kishirikina.
Je ni kweli wanawake wa kichaga(machame) huuwa waume zao...?
"Waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo laja"
Jambo hili liliniumiza kichwa na kujaribu kufanya utafiti wenye tija ya kutetea ni kweli wanawake wa kimachame huuwa waume zao au laa!!
Utafiti huu ulichukua takribani mwaka mmoja.
TAKWIMU...
Ni dhahiri kwamba kila baada ya kaya kumi utakuta wajane ndio wengine kuliko wagane: Namaanisa kwamba baada ya Nyumba kumi utakuta 6.4 ya kumi ni wajane. Je ni kweli wamachame huuwa waume zao? Twende pamoja kujua u kweli.
Nilijaribu pia kudodosa kwa wazee (majina nayahifadhi) kuhusu suala hili walinijibu vizuri na Leo napenda nawe ufahamu  Kwa nini wanaume wa kichaga hufa mapema kuliko wake zao? 
Ulishawahi kumtania mke wako hivi? Mke wangu unaonaje Tukauza lile shamba Tufanye biashara. Atakujibu Ukifa tulime wapi? ni dhahiri sisi wanaume tunatakiwa tufe mapema kuliko wao?
Muhuburi mmoja mashuhuri aliwali kusema nanukuu "wanawake wote duniani wanaamini wao hawafi mapema wanaoanza kufa ni wanaume" Mwisho wa kunukuu na wale mnaojua nguvu ya imani tumeelewa.


ZIFUATAZO NI SABABU ZA WANAUME WA KICHAGA KUFA KABLA YA WAKE ZAO...

1,MTINDO WA MAISHA..
Wanaume wa kimachame hupenda sana kutafuta hela, Utamkuta anaamka asubuhi mpaka jioni ni yeye na kazi tu. Na akipata hela anakuwa mbahili kiasi cha kutokujithamini kiafya kama kula vizuri na kuvaa pia. Jambo ambalo linawafanya kushinda na njaa kukonda na hata kupata magojwa kama vidonda vya tumbo Nk.
Jokes.. Ulishawahi muona mwanaume wa kichaga mnene? kama ndio ni unene wa mbeg...


2,KUOWA KWA KUCHELEWA..
Hapa ndo patamu, Kama wewe ni mchaga wa machame Ulishawahi kuangalia tofauti ya umri wa baba yako na mama yako?
Wanaume wa kichaga hawakuwa wanalipa suala la  kuoa kipaumbele wengi wao walikuwa wanasaka sana hela na maisha kwa ujumla, Jambo ambalo liliwapa kuja kuoa umri umeenda.
Baadhi yao walisaidiwa hata kuoa kwa nguvu na kushinikiziwa (kushikiwa mke). Jambo hili liliwapa wasaa Mdogo wa kufurahia ndoa yake kwani alifanya kuharakisha kuzaa watoto kwani umri umeenda. 
Pia ilichangia kufa mapema kwani akiwa na miaka 70  mke wake ana miaka 50.

3,LISHE DUNI..
Kilimanjaro ni mkoa wakopatikana Wachaga, Ni mkoa ambao unaweza kujiendesha wenyewe.
Kilimanjaro ni Kama bustani ya eden, Kwani udongo una rutuba mazao na nafaka ni nyingi zinazopatikana APA.
ubahili wa wachaga bwana, anaweza Lima mazao mengi ili apate hele na sio chakula. Ufahari wa mchaga hela bhana sio afya. Akila mboga mpaka aambiwe na daktari, maziwa anakamua Lita 10 yeye anatumia nusu lita tu. yaani akila kuku yeye au kuku mmoja wapo ni mgonjwa.
Ubahili wa kutokula mlo kamili hufanya mwili kudhoofika mapema na kukosa nguvu jambo ambalo hufanya  wanaume wa kimachame kufa kwa lishe duni kwa ubahili wao.

4,MATUMIZI YA POMBE..
Licha ya kutokula vizuri, Mchaga anamatumizi mabaya ya pombe (mbege) 
Mbege ni pombe ya ASILI ya Wachaga na hupendelea kuitumia baada ya kumaliza kazi kama pongezi na sehemu ya kujistarehesha na kuondoa uchovu.
Wanasayansi wanatuasa tuwe na matumizi ya kiasi katika pombe, huku makanisa na misikiti yakituasa tuache kabisa ni dhambi Ila mchaga na mbege hapana ni kama unampigia gitaa mbuzi tu.
Wanaume wa kichaga hunywa mbege sana kuliko kula anaweza akatoka shambani akaenda kilabuni kunywa mbege pasipo kupitia Nyumbani ale kwanza. Anauwezo wa kufanya kazi kubwa huku anakidumu cha mbege pembeni. Yaani mchaga na mbege humtoi.
Jambo hili limewapa sana wanaume kupoteza nguvu za kufanya kazi,kuishi na taifa kukosa watu wa kulijenga kwani wamekosa nguvu kabisa.
Matumizi ya mbege yamepuputisha sana maisha ya wanaume wengi wa kichaga.

5,UBAHILI...
Miongini mwa sifa kuu ya mmachame ni ubahili, Mchaga anauwezo wa kutembea kwa mguu umbali mrefu na ana hela mfukoni, Mchaga anauwezo wa kunywa chai  na andazi mchana ukapita. Mchaga anauwezo wa kununua Lita 2 ya mbege na sio maziwa. Yaani mchaga na ubahili ni Pacha tena wa kufanana.
Ubahili huu wa Wachaga umewafanya kutokujijali kiafya jambo ambalo linapelekea kwa wanaume kufa mapema.
Mwanaume wa kichaga anauwezo wa kwenda shambani na mbege kama chakula na akafanya kazi mpaka SAA kumi na moja jioni. 
Ubahili huu wa kutokujijali Ata ukiumwa ndio unaowauwa wanaume wa kichaga.
Mchaga mpaka akiri anaumwa ni alazwe na atundikiwe drop ya maji au damu LA  sivyo utamkuta shambani ama  dukani.
Jokes.. kuna mchaga aliumwa akalazwa alichofanya alipanda na gari lake akalipaki hospital akaka na funguo mpaka apone!

6,KAZI NGUMU...
Wanaume wengine wa kichaga hufanya kazi ngumu sana kama kulima na nyingine nyingi, Hupenda sana wanawake zao wabaki Nyumbani kuwasaidia kazi ndogo kama kupika.
Ufanyaji kazi wa mchaga huwa hauna mpangilio wa masaa  akienda shambani kitakacho mtoa ni Giza au mvua. Mchaga anafanya kazi ngumu na kwa masaa mengi jambo ambalo huwafanya pia kudhohofika kwani mda wote huo Ali chochote ZAIDI ya mbege na maji tu. Kweli mangi ataacha kutangulia?
jokes.. Ulishawahi kwenda dukani kwa mangi ukaambiwa ameenda kula? kama hayupo ni msalani kaenda..

7,SIKU ZA MAPUMZIKO...
Licha ya Mchaga kuongoza kwa kutafuta hela na kuimarika kiuchumi, Mchaga hanaga Siku ya mapumziko ZAIDI ya jumapili.
Muda wote mwanaume wa kichaga anawaza tu hela. Mchaga hawezi kutumia hela yake kuwatoa watoto out au mke wake Ata familia, mambo yote huwa ni uwakilishi tu mmoja abaki kazini.
Kama umempa kadi ya mwaliko mchaga yenye Mr&Mrs utaambulia Mr tu pasipo na Mrs au Mrs tu pasipo na Mr. atakuja mmoja huku mwingine akibaki kufanya kazi. 
Jokes... Ukimwalika mchaga sherehe ya usiku atakwambia ningekuja ila nani atanisaidia kukamua ngombe wangu?
Ndio maana sherehe nyingi za kichaga hufanyika mchana maana hutawapa muda mwingine.

8,PRESHA...
Wachaga walio wengi husumbuliwa na mshutuko wa moyo(PRESHA). 
Mchaga anapopanga mikakati yake ya kifedha au kiuchumi ikafeli hupata shida sana moyoni jambo ambalo huweza kuchukua Siku kadhaa akiliwazia. Mchaga akilima mazao yakaharibika huumwa kabisa. Mchaga akifungua duka akafilisika anapata presha.
presha ndio ugonjwa unaouwa sana wachaga. kustuka kwa mchaga Mara anapokosa shabaha yake ya kiuchumi ni kawaida.
jokes.... Ukitaka kumjua mchaga angusha sarafu chini tu utaona anavyoangaika kuona kama yake vile.


JE BADO UNAAMINI WANAWAKE WA KICHAGA NDIO WANAOUWA WAUME ZAO.
Yapo mengi sana yanayofanya wanaume wa kichaga kufa kabla ya wake ZAO. Nachowashauri wanaume wenzangu ni kwamba Tusiache kuoa machame,uchagani kisa tu dhana ya hii. kwamba wanawake wa kimachame  huuwa waume ZAO wanapotajirika. Suala hilo halina ukweli wowote.
Pia wachaga tuache ubahili tujijali tuweze kuishi miaka mingi  na kwa kufanya hivyo tutaweza kuwaaminisha wenzetu kuwa hatuuliwi na wake zetu kisa mali..

Nashukuru sana Mdau wangu wa blogi Yangu.
Pamoja na wazee walionipa ushirikiano katika hili mbarikiwe.
kwa lolote lile usiache kunicheki kupitia..

MAWASILIANO..
Facebook: SirGeorge Boaz
Instagram: officialsirGeorge
Google: MWALIMU GEORGE BOAZ
WhatsApp: +255621058168
SMS:+255621058168
S.L.P: 604Hai_Kilimanjaro
likee: SirGeorge Boaz
email: georgeboazndeyanka09 @gmail.com
UBARIKIWE SANA..




No comments:

Post a Comment

061058168