Tuesday, July 28, 2020

LIFAHAMU SALE JANI LENYE HESHIMA UCHAGANI.


LIFAHAMU SALE JANI LA KIMILA ZA WACHAGA.
Sale ni jani lililojizolea umaarufu mkubwa na heshima katika kabila la wachaga.
Vijana walio wengi wamekuwa na kukuta heshima na umaarufu wake ukipotea ndio maana niliamua kuwafahamisha japo kwa uchache kuhusu jani hili la sale.
Ukihudhuria sherehe nyingi za wachaga ukakuta wameliweka katika mdomo wa ndafu, Walio wengi huzani ni urembo au naksi flani katika ndafu kumbe laa!. 
Mwisho wa shamba (kyamba) mmoja na lingine LA mchaga huoteshwa. 
Sale ni jani lililopewa heshima sana na wachaga kuanzia Rombo,Tarakea,mashati,vunjo,old-moshi,kibosho,marangu,Machame na siha Na sehemu nyingine wanapokaa wachaga.
Kama mchaga akihamia ulipo mpakani lazima aoteshe sale.


YAFUATAYO NI MATUMIZI YA JANI SALE.
KUWEKA MPAKA..
Jani sale lilikuwa likitumika kama kuonyesha mwisho wa shamba(kyaamba) lako ni wapi ili usimwingilie jirani yako.

1,KUOMBA MSAMAHA...
Zamani jani la sale lilikuwa likitumika kuombea msamaha kwa makosa yaliyoonekana ni makubwa katika jamii za kichaga.
Ilikuwa mtu akija kukuomba msamaha uku ameshikilia jani la sale ni lazima umkubalie haikuwa na pingamizi maana ameonyesha kukiri kosa na kunyenyekea kwako kuomba msamaha.

2,KUFANYIA MATAMBIKO
Jani la sale pia lilikuwa likihusika katika mila za kichaga wakati wanapofanya matambiko yao. Walikuwa wakimwaga mbege chini huku majani ya sale wameyashika na mengine yapo chini. Madhabahu ya kufanyia matambiko yalikuwa sharti yawe na sale.

3,MAZIKO...
Jani la sale lilitumika pia kwenye  maziko, Wachaga walipomaliza hatua za kumpumzisha mpendwa wao waliweka majani ya sale juu ya kaburi ili kuweka alama kwamba apa amelala mpendwa wetu fulani. 

4,KUKARIBISHA MGENI..
Jani la sale limekuwa sehemu ya uchaga, Ilikuwa mgeni anapoingia katika boma la mchaga lazima apokelewe na vigelegele nderemo,shangwe na kupepewa na jani la sale wakiashiria ulipokuja ni salama hamna shari pia wamekubali ujio wako kwao.

5,KUTOA TAHADHARI...
Jani la sale na wachaga ni kama masai na ng'ombe, Mchaga alipoona sehemu kuna hatari kama vile shimo au sehemu panatitia waliweka apo jani la sale ili kuonyesha hapo sio sehemu salama usipite apo.

Licha ya umaarufu huo wa Jani LA sale halitumiki kama dawa ya ASILI.

kwa lolote lile usiache kunicheki kupitia..

MAWASILIANO..
Facebook: SirGeorge Boaz
Instagram: officialsirGeorge
Google: MWALIMU GEORGE BOAZ
WhatsApp: +255621058168
SMS:+255621058168
S.L.P: 604Hai_Kilimanjaro
likee: SirGeorge Boaz
email: georgeboazndeyanka09 @gmail.com
UBARIKIWE SANA..

No comments:

Post a Comment

061058168