Tuesday, May 18, 2021

KAMUSI YA KICHAGA SEHEMU YA PILI MAJINA YA VIUNGO VYA MWILI KWA KICHAGA NA MAANA YAKE

 Shamwindia ndee na maa, kwalolya na mashora. 

Shamwanaa denyi na ntiri ifugha lyevareiya ningi mbonyi teru ta kimashami. ando kulolya kutiri ulemi woi na woi ambaa daa. Kimaghuma kyelwekya isi vana wakoo lukuloshee na imanya kimashami nambo luidimie elosha na vana veghu.

ivuva kakwidimisia engera kulasare foo. kwengerie daa.


B, b

Bandama /bandama/ <li-> bandama: baba autwa ~ baba ametolewa bandama.

Biri /biri/ <ki-vi> kisogo: ~ ikee numa ya nghwe, Kisogo kipo sehemu ya nyuma ya kichwa.

E, e

Eeva/ɛɛβa/ <li-ya/ bega: ~ lyafika, bega limevunjika.ʊ

F, f

Fii /fii/ <u-zi> nywele: shikeuta ~ ninanyoa nywele.

Fiko /fikɔ/ <i-zi> figo: mwana alwee ~ mtoto anaumwa figo.

I, i

Ibusi /ibʊsi/ <i-zi> korodani: ng’umbe yaghumbuwa ~ ng’ombe amekatwa korodani

Ifua /ifʊa/ <u-zi> mfupa: afika ~ lya eeva, amevunjika mfupa wa bega.

Ifua lya mbwa/Ifʊa lja mbwa/ <u-i> mfupa wa pua: ~ lyikee lyuumu den fo, mfupa wa pua sio mgumu sana.

Ifua lya ng’ang’ani /ifʊa lja ŋaŋani/ <u-> uti wa mgongo: ~ lyafika, uti wa mgongo umevunjika.

Ifua lya si/ifʊa lya si/ nm <u-i> mfupa wa maungo ya chini: marende alungywe ~ miguu imeungwa kwenye mifupa ya maungo ya chini.

 

 

Ikekele /ikɛkɛlɛ/ <li-ya> kwapa: ~ lyitiri fii shiingi, kwapa lina nywele nyingi.

Ikoro /ikɔrɔ/ <li-> koromeo: amanywa~ amekatwa koromeo.

Ilungo lya singo<ilʊŋgɔ lya siŋgɔ/ nm <u-zi> pingili ya shingo: ~ lyeeghuka, pingili ya shingo imeteguka.

Iongosho /iɔŋgɔ∫ɔ/ <i-zi> kongosho: alelwaa ~ kafwa, aliumwa kongosho akafa.

Irima /iɣima/ <li-ya> ini: nyama ya ~ irola den, nyama ya ini ni tamu sana.

Iriso /iɣisɔ/ <li-ya> Jicho: ~ likeuta misoru, jicho linatoa machozi.

Itaari /itaaɣi/ <li-ya> paja: ~ lyakwa llyisise, paja langu ni jembamba.

Ivashivashi /׀βa∫iβa∫i/ nm <li-ya> pafu (mapafu): ~ lya nndu lyikaishwa mura kuti afwe, mapafu ya mtu yakijaa maji lazima afe.

Ivee /iβɛɛ/ <li-ya> ziwa, titi, nyonyo: nka ulya atiri ~ lyimwi, yule mwanamke ana ziwa moja.

Iyoo /Ijɔɔ/ nm <li-ya> jino: ~ lya mwana lyikeiluwa ndesi, jino la mtoto litangolewa kesho.

Iyusi /iɲʊsi/ <u-zi> nyusi: akeuta ~ ananyoa nyusi.

K, k

Kana /kana/ <u-i> kinywa, mdomo: ambira ~ kinywa, panua mdomo kidogo.

kibobosho /kibɔbɔ∫ɔ/ kitovu: mwana aghumbuwa ~ mtoto amekatwa kitovu.

Kidari /kidaɣi/ <ki-vi> kidari: atiri ~ kiniini, ana kidari kikubwa; vika ~ mbee, weka kidari mbele.

Kidudu /kidʊdʊ/ <u-> uume: mwana atiri ~ kinywa, mtoto ana uume mdogo.

Kilumi /kilʊmi/ <ki-vi> kilimi: ~ kikee kufi na ikoro, kilimi kipo karibu ya koromeo.

Kinenaa /kinɛna/ <ki-vi> kinena: ~ kikerera.

Kinena kinawasha.

Kinu /kinʊ/ <u-> uke: ~ kya nkyeku, uke wa mzee.

Kinyinyi /kiɲiɲi/ <u-> fizi: mwana atiri ~` filini, mtoto ana fizi laini.

Kiromu /kirɔmʊ/ <u-i> mdomo: ~ kya uwe nkiniini ngota kya si, mdomo wa juu ni mkubwa kuliko wa chini.

Kisaa /kisaa/ <li-ya> matako: vika ~ ghembo, kalasha matako chini.

Kisangu / kisaŋgʊ/ <u-zi> uso: ~ kyakwe kifani, uso wake ni mchafu.

Kishengele /ki∫ɛŋgɛlɛ/ <ki-vi> kifundo cha mguu: aumya ~ akeidima eenda fo, ameumia kifundo cha mguu hawezi kutembea.

Kishengele /kiʃɛŋgɛlɛ/ nm <ki-vi> kifundo cha mguu: ~ kikevava, kifundo cha mguu kinauma.

Kisi /kisi/ <ki-vi> kiuno: runguta ~ mpaka si,

Kisima /kisima/ kisima: mwana amanywa ~ mtoto amekatwa kisima.

Kiwiliwili /kiwiliwili/ <ki-vi> kiwiliwili: ~ kitiri mafua meengi den, kiwiliwili kina mifupa mingi sana.

Kyeeri /kjɛɛɣi/ <ki-vi> kidevu: ~ kya nka kitiri nguyo, kidevu cha mwanamke kina ndevu.

M, m

Mafua a uwe/mafʊa aʊwɛ/ nm <u-i> mifupa ya maungo ya juu: ~ akulungye kisha, mifupa ya maungo ya juu umeunganika vizuri.

Mbafu/mbafʊ/ <ki-vi> kifua: mf, mbafu ikebara, kifua kinauma.

Mbari /mbaɣi /nm <i-zi> mbavu: awa kafika ~ shikoo, ameanguka akavunjika mbavu changa.

Mbava ta iriso/mbaβa ta iɣisɔ/ nm <i-zi> kope: ~ tighingaa miso, kope hulinda macho.

Mbwa /mbwa/ nm <i-zi> pua: ~ ifaamyaa, pua inatumika kunusa; ~ ing’ani, pua ni kubwa.

Mfiko wa imamu/mfikɔ wa imamʊ/ nm <ki-vi> kibofu cha mkojo: ~ udoroshukye, kibofu cha mkojo kimetoboka.

Mini ta marende/mini ta maɣɛnde/ nm <ki-vi> vidole vya miguu: ~ tiifo ikumi, vidole vya miguu vipo kumi.

Mungo /mʊŋgo/ nm <u-i> mgongo: lema ~ kunja mgongo; vika mwana ~ beba mtoto mgongoni.

N,n

Ndeu /ndɛʊ/ nm <li-ya> tumbo: ~ ikevava den, tumbo linauma sana.

Ndi /ndi/ nm <li-ya> goti: firya ~ piga goti; orwa ~ nyoosha goti.

Ngala /ŋgala/ nm <i-zi> kucha: vyaa ~ kata kucha; ebikya ~ fuga kucha.

Ngoma ya kuri/ŋgɔma ja kʊɣi/ nm <i-zi> ngoma ya sikio: ~ yabarika, ngoma ya sikio imepasuka.

Ngoo /ŋgɔɔ/ nm <u-i> moyo: ~ ikekaba kwa finya, moyo unadunda kwa kasi.

Ngosi/ŋgɔsi/ nm <i-zi> ngozi: ~ itiri mafwaa, ngozi ina vinyweleo; ~ yampaluka, ngozi imepauka.

Ngoso /ŋgɔsɔ/ nm <u-I> mkundu: ~ ikeuta samu, mkundu unatoa damu.

Ngushu /ŋgʊ∫ʊ/ nm <li-ya> shavu: fumba~ vimba shavu; tira ~ shika shavu.

Nguyo /ŋgʊjɔ/ nm <i-zi> ndevu: uta~ nyoa ndevu; mmya~ ota ndevu.

Nni /nni/ nm <ki-vi> kidole: orwa ~ nyoosha kidole; lema ~ kunja kidole.

Nnrwe /ŋɣwɛ/ nm <ki-vi> kichwa: ~ wa mwana, kichwa cha mtoto; ~ ukebara, kichwa kinauma.

Nraari /ŋɣaaɣi/ nm <u-i> mshipa: ~ ukeita samu shiingi, mshipa unapitisha damu nyingi.

Nshesha /nʃɛʃa/ nm <u-> uroto: ifua lyitiri ~ nshesha mfumbutu den, mfupa una uroto mwingi sana.

Nyinyiri ya iriso/ɲiɲiɣi ja iɣisɔ/ nm <i-zi> mboni: ~ yaangiswa, mboni imechafuka; finga ~ fumba mboni.

Nyusi /ɲʊsi/ nm <u-zi> nyusi: illwa ~ ng’oa nyusi; songosya ~ tinda nyusi

O, o

Oko /ɔkɔ/ nm <u-I/ mkono: ~ lukee lwaasha, mkono mrefu; ~ lwa birika, mono wa birika.

S, s

Samu /samʊ/ nm <i-> damu: mwana aanguywa ~ mtoto amepungukiwa damu.

Shonyi /ʃↄɲi/ nm <i-zi> ngozi: ~ ya ng’umbe ifani shuu, ngozi ya ng’ombe ni nyeusi.

Shoro /ʃↄrↄ/ nm <li-ya> paja: ~ ikerera, linawasha.

Singo /siŋgↄ/ nm <i-zi> shingo: ~ ikerunguka, shingo inazunguka.

T, t

Tutu /tʊtʊ/ nm <ki-vi> kisigino: ~ itiri maanga, kisigino kina magaga.

U, u

Udwa /ʊdwa/ nm <i-zi> nyonga: ~ lwaengereka, nyonga imetanuka.

Ukokwa /ʊkↄkwa/ nm <ki-vi> kiwiko: akabwa ~ lwa kisangu, amepigwa kwa kiwiko usoni.

Ulumi /ʊlʊmi/ nm <u-zi> ulimi: ~ lukeonsha shumbi na sukari, ulimi huonja chumvi na sukari.

Urende /ʊꙋɛndɛ/ nm <u-i> mguu: nsee akeorwa ~ kijana ananyoosha mguu.

Urongo /ʊrↄŋↄ/ nm <u-zi> ubongo: mwana atiri ukiva lwa ~ mtoto ana matatizo ya ubongo.

Uroro /ʊꙋↄꙋↄ/ nm <u-> utosi: ~ wa mwana ukee nkoo, utosi wa mtoto ni mchanga.

Utumbo lusiise/ʊtʊmbↄ lʊsiisɛ/ nm <u-ya> utumbo mwembaba: ~ lukee lwaasha ngota utumbo unini, utumbo mwembamba ni mrefu kuliko utumbo mpana.

Utumbo unini/ʊtʊmbↄ ʊnini/ nm <u-ya> utumbo: mama alwee ~ unini mama anaumwa utumbo mpana.

Uvayo /ʊβajↄ/ nm <u-zi> unyayo: ~ lukevaria kila ando, unyayo unakanyaga kila mahali.

Uwengu /ʊwɛŋgʊ/ nm <i-zi> 1 bandama: ~ lyabarika, bandama imepasuka. 2 kongosho: ~ ikee kufii na ndeu, kongosho iko karibu na tumbo.

Y, y

Yaarwi /jaaꙋwi/ nm <li-ya> sikio: ~ lyiitye foo, sikio halisikii.

Yuundu /jʊʊndʊ/ nm <li-ya> gego: ~ lyikevava, gego linauma.

zungusha kiuno hadi chini.

MAWASILIANO



Facebook: SirGeorge Boaz

Instagram: officialsirGeorge
Google: MWALIMU GEORGE BOAZ
WhatsApp: +255621058168
SMS:+255621058168
S.L.P: 604Hai_Kilimanjaro
likee: SirGeorge Boaz
email: georgeboazndeyanka09 @gmail.com
UBARIKIWE SANA..

No comments:

Post a Comment

061058168