Monday, June 7, 2021

KARIBU TANGA WAJA LEO WAONDOKA LEO.

KARIBU TANGA:

Waja leo waondoka leo.

Na mwandishi  GEORGE BOAZ.


Tanga ni moja ya mikoa inayounda nchi ya Tanzania, Mkoa huu unapatikana kaskazini mwa Tanzania. Tanga ni moja ya mikoa yenye historia ya kipekee sana nchini Tanzania, Mkoa huu umeundwa na wilaya 10 (kumi) huku ukikadiriwa kuwa na km 27,348  na makao makuu  yake yakiwa ni Tanga mjini.

Tanga insaemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 BK. Tanga ni mji ambao sifa zake zilianza kusikika kuanzia enzi za utawala wa Wajerumani, jiji ambapo shule ya kwanza ya serikali ilijengwa enzi hizohizo za utawala wa Wajerumani, jiji ambalo liliendelea kukua sana kutokana na kilimo cha katani na hivyo kukusanya vijana toka kila kona ya nchi kuja kutafuta kazi katika mashamba makubwa ya katani wakati huo.

Tanga ni moja pia ya mikoa ulio fukoni mwa Bahari ya Hindi wenye Postikodi namba 21100.

Tanga ndio mkoa pekee unaosifiwa kuwa ndiko mapenzi yalipozaliwa  je? Ni ya kweli, Tuambatane katika makala hii fupi kuhusu Tanga.

Yaliyomo:

·         HISTORIA YA TANGA.

·         USAFIRISHAJI.

·         UTALII.

·         KILIMO NA VIWANDA.

·         WAKAZI.

·         ENEO.

·         SANAA.

·         MENGINEYO.

HISTORIA YA TANGA:

Kama tulivyokwisha kutazama kwa uchache historia ya mkoa wa Tanga hapo juu. Tanga ni mkoa wenye historia ya kipekee katika Nyanja zote. Tukisema tuelezee muda hautatosha kwa maana ni hadithi ndefu kusimulia.

Tanga ni Jina la mji wa Tanga linaaminiwa kutokana na lugha ya Kibondei yaani Shamba, kwa sababu wenyeji ambao walikuwa Wabondei waliishi kisiwa cha Toten lakini shughuli zao za kilimo walizifanyia eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama mji wa Tanga.

 

USAFIRISHAJI:

Katika suala la ubebaji na usafirishaji Tanga imebarikiwa kuwa na aina zaidi ya tatu za usafirishaji. Tunaweza sema jiji la tanga ni moja ya mikoa ambayo unaweza kufika kwa njia mbalimbali.

Kwanza Tanga ina usafirishaji wa barabarani unaounganisha mkoa wa Kilimanjaro na wa pwani kupitia same na korogwe. Pili ni usafirishaji wa njia ya reli unaotoka Tanga kwenda Kilimanjaro mpaka Arusha, na tanga kwenda Dar es salaam kupitia Pwani. Tatu ni usafirishaji wa anga unaotoka kiwanja cha ndege tanga kwenda viwanja vingine vya ndege. Nne ni usafirishaji wa majini ukihusisha Bandari ya KASELA tanga inayotoa huduma kwenda bandari nyingine kama bandari ya dar e s salaam

 

UTALII:

Mkoa wa Tanga una maeneo ya kitalii yanayoweza kuwavutia watalii wengi ndani na nje ya Tanzania, Hasa kutokana na ukarimu wa watu wake. Watu wa Tanga wanasifika kuwa na haiba ya ukarimu kama walivyo watanzania wengi jambo ambalo linaweza kuwa kivutio kwa watalii wengi kutembelea mkoa huo. Kwa kawaida ukarimu huwavutia watalii wengi, Na kuwajengea hali ya usalama na kujifunza mengi kutokana kwa wenyeji wao.

Mkoa wa tanga umebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo husaidia katika kukuza pato la Nchi na la mkoa huo. Mbali la pato vivutio hivyo husaidia kuleta fedha za kigeni na kuufanya mji huo kukua. Mojawapo ya vivutio hivyo ni Amboni caves, kisiwa cha Toten, Magofu ya Tongoni, Kisiwa cha ulenge, Sakarani makaburi ya vita kuu ya kwanza ya dunia, Mbuga ya wanyama saadani, Mto pangani, Msitu wa Magoroto,  Mbuga ya mkomanzi,  Urithi  Tanga museum na fukwe za bahari zenye upepo mwanana.

 

KILIMO NA VIWANDA:

Kama ilvyo kwa mikoa mingine hapa Tanzania hulima ndivyo ilivyo kwa mkoa wa Tanga, Tanga hutegemea kilimo cha riziki, uvuvi na ufugaji.

Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. Kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.

Mkoa wa Tanga ulikuwa na viwanda vingi sana hii ni kutokana na kuwa katika ukanda wa pwani ambapo watu toka magharibi waliweza kufikia hapo kwa haraka kuliko mikoa mingine ya Tanzania, Ujio wa watu wa magharibi walifanya jiji la Tanga kukua haraka na kuwa na viwanda vingi vyenye kuzalisha bidhaa mbalimbali kama vile, Saruji, Mafuta ya kupakana bidhaa nyinginezo nyingi.

Pia mkoa wa Tanga umekuwa maarufu kwa umekuwa maarufu kwa kilimo cha Mkonge na matunda matunda pia kuna viwanda vya uchakataji wa mkonge na usindikaji wa matunda.

 

WAKAZI:

Mwaka 2012 wakazi waliohesabiwa katika sensa walikuwa 2,045,205[1].

Makabila makubwa mkoani Tanga ni WasambaaWaziguaWabondei na Wadigo. Mengine ni WapareWataitaWambuguWasegeju na Wanago.

Pia kuna Waarabu wengiwengi wenye asili ya Oman.

Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milima ya UsambaraMuhezaKorogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.

Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga yenyewe na sehemu za pwani.

ENEO:

Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake. Msongamano ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto kwenye ardhi yenye rutuba nzuri.

Mkoa una eneo la km² 27,348 ambalo linaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.

Eneo linalofaa kwa kilimo ni km² 17,000.

Kuna wilaya 10 ambazo ni Handeni VijijiniHandeni MjiniKilindiKorogwe VijijiniKorogwe MjiniLushotoMkingaMuhezaPangani na Tanga Mjini.

SANAA:

Nanukuu; “Tanga ni mji ambao sifa zake zilianza kusikika kuanzia enzi za utawala wa Wajerumani, jiji ambapo shule ya kwanza ya serikali ilijengwa enzi hizohizo za utawala wa Wajerumani, jiji ambalo liliendelea kukua sana kutokana na kilimo cha katani na hivyo kukusanya vijana toka kila kona ya nchi kuja kutafuta kazi katika mashamba makubwa ya katani wakati huo.

Tanga ni mji ambao kutokana na wingi wa vijana wakati huo, shughuli za burudani ya muziki nazo zilifikia kiwango cha juu kuliko sehemu nyingi Tanzania.

Ukizungumzia historia ya muziki wa dansi, huwezi kukwepa kuzungumzia Tanga, kwani historia inatueleza kuwa kabla ya kuanza vikundi vya muziki wa dansi kulianzishwa klabu za kucheza dansi. Klabu hizo zikitumia muziki wa santuri, wanachama wake walicheza na hata kushindana kucheza muziki kwa mitindo mbalimbali ya kigeni ikiwemo waltztangochacharumba na kadhalika.

Klabu za kwanza nchini zilianzia Tanga. Kulikuwa na klabu kama Young Noverty miaka michache baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia, wakati huo nchi ya Tanganyika ikiwa bado changa kabisa. Mtindo huu wa vilabu vya dansi ulienea na baadaye kuingia Dar es Salaam na miji mingine iliyokuwa imeshaanza wakati huo. Vilabu hivi ndivyo baadaye vilivyanzisha vikundi vya kwanza vya muziki wa dansi. Hata majina ya vikundi hivyo vya kwanza yalihusiana na klabu za burudani za wakati huo. Kulikuwa na vikundi kama Coast Social Orchestra, Dar es Salaam Social Orchestra na kadhalika.

Hivyo mji wa Tanga ulikuwa katika ndoto za vijana enzi hizo. Kwa vile vijana wengi walikusanyika katika jiji hilo, kulianzishwa pia klabu ambazo zilikuwa kwa ajili ya vijana waliokuwa wakitoka kabila moja. Klabu hizo zikiwa na nia ya wanachama wao kusaidiana katika shida na raha, na vilabu hivyo pia vilikuwa sehemu muhimu katika kutoa burudani kwa vijana waliotoka sehemu moja.

Kati ya klabu hizo kulikuweko na klabu iliyoitwa Young Nyamwezi: kama jina lake lilivyo ilikuwa klabu ya vijana kutoka Unyamwezi. Hatimaye mwaka 1955 klabu hiyo ilianzisha bendi yake iliyoitwa Young Nyamwezi Band, bendi hiyo ilikuja kukua na baada ya uhuru ilibadili jina na kuitwa Jamhuri Jazz Band. Hakika kwa vijana waliokuwa wapenzi wa muziki miaka ya 1960 na 1970 ilikuwa lazima uifahamu Jamhuri Jazz Band, muziki wake, au kwa lugha ya enzi zile, ‘vibao’ vyake vilivyojulikana Afrika ya Mashariki nzima. Bendi hiyo ilikuwa ikibadili mitindo ya upigaji wake na kupiga katika mitindo ya ‘Toyota’ na hatimaye ‘Dondola’. Aliyekuja kumiliki bendi hiyo, ambayo wapenzi wake pia waliita JJB alikuwa Joseph Bagabuje, kulikuwa hata maelezo wakati fulani kuwa JJB ilikuwa kifupi cha Joseph Jazz Band na si Jamhuri Jazz Band. Kama ilivyokuwa kawaida ya bendi za wakati ule Jamhuri Jazz Band ilisafiri sana na kufanya maonyesho katika kila kona ya nchi, jambo hilo pamoja na kuwa bendi hii ilirekodi na kutoa santuri kupitia kampuni za kurekodi za Kenya na pia kurekodi nyimbo zake katika radio ya Taifa uliifanya bendi hiyo kuwa maarufu sana.

Upigaji wa aina ya pekee wa gitaa la rhythm wa bendi hii, ambao uligunduliwa na Harrison Siwale, maarufu kwa jina la Sachmo, uliigwa na wapiga gitaa ya rhythm wengi nchini. Uimbaji wa kutumia waimbaji wawili tu, uliopendelewa na bendi za Tanga wakati huo ikiwemo bendi nyingine maarufu ya Atomic jazz Band, ulikuwa wa aina yake pia.

Jamhuri Jazz Band pia ndiyo ilikuwa chanzo cha bendi maarufu ya Simba wa Nyika. Inasemekana kuwa siku ambayo Jamhuri Jazz Band ilikuwa imekodishwa kwa ajili ya kupiga kwenye harusi kule MuhezaWanamuziki walikuwa wakilazimika kukusanyika katika jengo la klabu lililokuwa Barabara ya 15 ili kupata usafiri wa kwenda Muheza. Siku hiyo wanamuziki wengine walikusanyika lakini George na Wilson Peter, Luza Elian na wengine wachache hawakuonekana. Baada ya upelelezi mfupi ikajulikana kuwa wamejificha au wameondoka mjini Tanga, hivyo ikalazimika kutafuta wanamuziki viraka wa harakaharaka kuweza kufanikisha onyesho la siku hiyo.

Kwa karne hii ya 21 Tanga pia inao wasanii maarufu ndani na nje ya Tanzania wanaojulikana maarufu kama   Sumalee, Cpwaa{halifa ilunga}, Matonya{Sefu Shabani}, Kassim Mganga, Wagosi wa Kaya, Ring 2be aka Pete{Rashidi Ngayama},  Mwana FA{Hamisi Mwinjuma}, Bwana Misosi, Q Chilla{Abubakari Katwila}, MB Doggy, R.O.M.A{Ibrahim Mussa}, Top C, Dr Karim, John Walker,  Gelly wa rhym, Hemed Phd{Hemed Suleiman}, Sharomillionear{Mohamed Mtikey},Danny Msimamo  Pia waigizaji maarufu kama  hayati King  MAJUTO  walitokea mkoa waTanga.

Tanga na mapenzi ni hadithi isiyoweza simulika pasi na kupata wasaa wa kuonya utamu huu kwa kuishi katika jamii hii au kuoa/kuolewa tanga kwani wahenga walisemaa raha ya ngoma uingie ucheze.

Kutokana na maelezo hapo juu kuhusu simulizi ya mkoa huu, Vijana wengi walivyopenda kwenda tanga kwani ndio mji uliokuwa umeendelea na ulikuwa na ustaarabu wa magharibi ulifanya suala la mapenzi  kuongezeka. Hii ni kutokana na mwingiliano wa makabila pia uwepo wa utamaduni wa ngambo(wazungu na waarabu)

NB: Wakenya  huwa na msemo wa Mombasa raha,  na ukija ukiangalia kijiografia Mombasa na Tanga imepakana na zote zipo uwanda wa pwani.  Kuwepo kwa starehe na burudani kiasi cha kusifiwa ni matokeo ya Miji hiyo kuendelea mapema kabla ya mingine huku ikiwa na miingiliano ya tamaduni toka ndani na nje ya mipaka yake. Pia kuwepo na ustaarabu wa ngambo ya magharibi.

MENGINEYO:

Salamu maarufu ya wakazi wa Tanga ni

NENO

TAFSIRI

1.       Assalam Alaikum

Amani iwe na wewe

2.       Onga makeo

Habari za asubuhi. (kisambaa)

Kutokana na Tanga kuwa na makabila zaidi ya moja uwepo wa salamu mama hamna. Zaidi hutumia salamu ya dini ya kislamu kutokana na wakazi hao wengi kuwa wafuasi wa  dini hiyo.

Bwana yesu asifiwe ni chache hivyo  unaweza kutumia lugha ya taifa kutoa na kuitikia salamu.

 


 Facebook: SirGeorge Boaz

Instagram: officialsirGeorge
Google: MWALIMU GEORGE BOAZ
WhatsApp: +255621058168
SMS:+255621058168
S.L.P: 604Hai_Kilimanjaro
likee: SirGeorge Boaz
email: georgeboazndeyanka09 @gmail.com
UBARIKIWE SANA..

No comments:

Post a Comment

061058168