Monday, July 4, 2022

JE! LUGHA YA WACHAGA NI MOJA?

 LUGHA YA WACHAGGA NI MOJA.

– Kumekuwa na Utata wa Muda Mrefu Kuhusu Kama Wachagga Wanaongea Lugha Moja Au Ni Lugha Mbalimbali Tofauti, Jambo Ambalo Limeleta Utata Mwingine wa Kwamba Kama, Je Wachagga Ni Jamii Moja Au Ni Jamii Mbalimbali Zilizojikuta Zinaishi Kwenye Mlima Kilimanjaro na Kuamua Kujiita Kwa Pamoja Wachagga?

– Jibu Ni Lugha Ya Kichagga ni Moja, Lakini Ikiwa Katika Lahaja Mbalimbali za Kichagga. Wachagga Ni Jamii Moja Iliyogawanyika Katika Himaya Mbalimbali na Lahaja Mbalimbali Za Lugha Moja Kuu Ya Kichagga.

– Swali Lingine ni Je, Kwa Nini Kuwe na Lahaja Mbalimbali Kusiwe na Lugha Moja Tu Ya Kichagga Kama Ni Jamii Moja?

– Tunasema Kichagga ni Lugha Moja kwa Sababu Mwanzoni Kabisa Kulikuwa na Lugha Moja Ya Kichagga Inayofanana kwa Kila Kitu Ambayo Ilikuwa Inazungumzwa na Wachagga Wote Kilimanjaro Wakati Wachagga Wanahamia Kilimanjaro Wakiwa Kama Jamii Moja.

– Baada Ya Kuishi Kilimanjaro kwa Muda, Watu wa Jamii Nyingine Kutoka Nje Ya Kilimanjaro Walianza Kuhamia Kilimanjaro kwa Kasi Kuungana na Wachagga Waliokuwa Wanaishi Kilimanjaro. Watu Hawa Waliotokea Pande Mbalimbali za Kilimanjaro Ambao Waliingia kwa Makundi Madogo Madogo Ndio Walisababisha Lugha Halisi Ya Wachagga Kuendeleza Utofauti Uliotokea Kati Ya Eneo Moja na Jingine Kwa Sababu Walikuwa Wengi Kiasi.

– Wingi wa Watu Waliohamia Kilimanjaro Kuungana na Wachagga Walitokea Upande wa Mashariki Ambao Kwa Sehemu Kubwa Leo Hii Ni Nchi Ya Kenya Ambapo Zaidi Walitokea Jamii za Wataita na Wakamba na Wamasai Pia. Eneo Lilioathirika Zaidi na Mwingiliano Huu Kuliko Maeneo Mengine Yote ni Eneo La Rombo, Hasa Upande wa Mashariki Zaidi. Lakini Hata Upande wa Magharibi wa Uchagga Waliingia Kiasi Wamasai Lakini Sio kwa Wingi Kama Mashariki.

– Kwanza Inajulikana Kwamba Eneo La Katikati Ya Uchagga Kuanzia Uru, Old Moshi na Vunjo Yote(Maarufu Kama Marangu) Mpaka Mwika Wanaongea Lugha Moja kwa Karibu Asilimia 100%, Huku Eneo La Vunjo Peke Yake Wakiongea Lugha Moja kwa Asilimia 100%, Huku Kibosho Nayo Lugha Ikiendana na Eneo Hili La Katikati Ya Uchagga kwa Zaidi Ya 80%, na Hata Karibia Nusu Ya Rombo Kuanzia Mamsera Mpaka Mkuu Lugha Ikikaribiana Sana na Hili Eneo La Katikati Ya Uchagga.

– Upande wa Magharibi Kabisa na Upande wa Mashariki Kabisa Ndio Lugha Inakaribiana Kwa Asilimia Kama 60% – 70% Peke Yake, Lakini Bado Ukifuatilia Vizuri Utakuta Aidha Asili Ya Maneno Mengi Ni Yale Yale, Au Utakuta Kuna Maneno Mbadala Ambayo Yanafanana Au Yanakaribia Kufanana Na Ya Hili Eneo La Katikati Ya Uchagga.

– Kwa Mfano, Neno “Nyumbani” Kwa Wachagga wa Hili Eneo La Katikati Wanasema “Kanyi”, Ukienda Machame Japo Nyumbani Imezoeleka Kama “Boo” Lakini Neno Lingine Mbadala La Tafsiri Ya “Nyumbani” Ni “Kenyi” Ambalo Linafanana Tena Kidogo na Neno “Kanyi” Linalotumiwa na Wachagga Wa Eneo La Katikati Kumaanisha Nyumbani.

– Mfano Mwingine Ni Neno “Chakula” Ambalo Kwa Wachagga wa Hili Eneo La Katikati Wanaita “Kyelya”, Ukienda Machame Japo Chakula Wanaita “Shonga”, Lakini Wakisikia Kyelya Wanaelewa Ni Chakula.

– Hivyo Tunasema Kwamba Lugha Ni Moja Kwa Sababu Kwa Sehemu Kubwa Inafanana, na Kwa Yale Maeneo Yenye Utofauti Utakuta Aidha Ni Utofauti Wa Utamkaji, Au Kuna Msamiati Mbadala Unaoendana na Kichagga cha Eneo La Katikati, Au Kuna Msamiati Ulishasahaulika Zamani Uliokuwa Unaendana na Kichagga cha Eneo Katikati Ya Uchagga. Hivyo Inabaki Kwamba Asili Ya Lugha Ni Moja na Huo Mgawanyiko Ni Lahaja Tu Za Lugha Kuu Moja Ya Kichagga.

Suala La Jamii Moja Kuwa na Lahaja Nyingi za Lugha Kuu(Dialects) Sio Jambo La Ajabu Au Jambo La Wachagga Peke Yao. Hili Tunaweza Kuliona Pia kwa Uyunani Ya Kale Ambao Walikuwa Ni Jamii Moja Lakini Iliyogawanyika Kama Walivyo Wachagga Ambapo Kulikuwa na Wayunani wa Athene, Wayunani wa Spata, Wayunani wa Korintho, Wayunani wa Thebe, Wayunani wa Sirakusa, Wayunani wa Makedonia, Wayunani wa Egina, Wayunani wa Rodo, Wayunani wa Eretria n.k.,.

– Wote Hawa Walikuwa Ni Jamii Moja Ya Wayunani Lakini Waliokuwa Wamegawanyika Katika Himaya Ndogo Ndogo Nyingi na Licha Ya Kwamba Walikuwa na Lugha Moja Ya Kiyunani Lakini Ilikuwa Katika Lahaja Mbalimbali za Kiyunani.Wayunani Walikuwa Ni Wasomi, Wanasayansi, Wanafalsafa, Watawala, Wafalme Wakuu na Watu Mashuhuri Sana wa Dunia Ya Kale, Hata Licha Ya Kwamba Harakati za Dini Ya Kikristo Zilianzishwa na Watu wa Asili Ya Kiyahudi Lakini Biblia Ya Kwanza kwa Upande wa Agano Jipya Iliandikwa kwa Kiyunani cha Lahaja Ya “Koine” Kwa Sababu Ndio Iliyokuwa Lugha Ya Wasomi na Watu Mashuhuri kwa Nyakati Hizo, Ambapo Hata Alexander Mashuhuri(Alexander the Great) Alikuwa ni Myunani, Wakati Huo Wayahudi Wakiwa ni Watu wa Hadhi Ya Chini Ambao Hata Lugha Yao Haikuwa Imejitosheleza Sana Kimaandishi na Isiyo na Heshima Kubwa.

– Hata Biblia Ya Kwanza Ya Agano La Kale Ya Kiyahudi “Septuagint” Iliyoandikwa Kwa Ajili Ya Wayahudi(Waisrael) Wakiwa Uhamishoni Misri Nyakati za Ptolemi Iliandikwa Kwa Kiyunani cha Lahaja Ya Koine.

– Hivyo Lugha Kuu Ilibaki Kuwa ni Kiyunani Lakini cha Lahaja Fulani, na Sio Lahaja Kugeuka Kuwa Lugha Kuu.

– Kwa Mujibu wa Mary Kathleen Stahl, Mmoja Kati Ya Wanahistoria Maarufu wa Kichagga, Kutokana na Mapinduzi na Mabadiliko Makubwa Ya Kisiasa Yaliyokuwa Yanaendelea kwa Wachagga Karne Ya 20, Lugha Ya Kichagga Ilikuwa Imeanza Kubadilika Taratibu Kuelekea Kuwa Moja Tena na Endapo Mwenendo wa Mambo Ungeendelea Vile Vile Kama Ulivyokuwa Unaenda Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika Wachagga Wangerudi Tena Kwenye Lugha “Standard” Moja Ndani Ya Kipindi cha Miaka 30 Mpaka 50.

– Mangi Mkuu wa Wachagga Thomas Lenana Marealle Alitaka Kuharakisha Zoezi Hili kwa Kurasimisha Lugha Ya Kichagga Miaka Ya 1950’s, na Kwa Kuanza Alitaka Magazeti Ya Wachagga Yaandikwe kwa Lugha Ya Kichagga na Lugha Ya Kichagga Iendelee Kutumika Baadhi Ya Maeneo Kama Lugha Rasmi, Kama Walivyofanya Kanisa La Kilutheri. Hata Hivyo Mangi Mkuu Alikutana na Changamoto Kiasi Kutokana na Kutokuwa na Sauti Ya Mwisho na Hivyo Utekelezaji Wake Ukafifia Kidogo Miaka Ya Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika.

MAWASILIANO


Tell+255 621 058168=whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com


Google: Mwalimu george boaz 

facebook: sirGeorge Boaz 

HAI

KILIMANJARO

Sunday, March 6, 2022

MZEE WA KICHAGA AKIASA VIJANA KUOA


 MAWASILIANO


Tell+255 621 058168=whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com

Google: Mwalimu george boaz 

facebook: sirGeorge Boaz 

HAI

KILIMANJARO

Saturday, August 21, 2021

Video ya salamu za kichaga

Bofya hapo chini kutazama na kusikiliza video ya salamu ya kichaga






MAWASILIANO

Tell+255 621 058168=whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com

Google: Mwalimu george boaz 

facebook: sirGeorge Boaz 

HAI

KILIMANJARO

UTANI WA WACHAGA

Leo napenda kuwapa utani wa wachaga: Please usikasirike ni utani tu wenzangu.


 

ü  WAROMBO:

Warombo ni wajanja sana kibiashara/wezi pia, wanapenda dili za magendo mno. Ni walevi sana kuliko ma wachaga wengine, huwapeleka wake zao kijijini wanapoleta kujua mjini. Wanaume wa rombo wanachunwa sana na wanawake wa marangu na wanawaita “Vishohia”  

Wanawake wa rombo ni mama huruma sana huwa hawakatai. Ukioa mrombo ujue umeolea wenzako.

Wanaume wa rombo hawawezi kuridhisha wapenzi wao jambo linalopelekea kuchepuka na kuomba msaada/Jeshi la uokoaji na unusuruji wa ndoa Kenya.

Ni utani tu wenzangu Warombo ila mbadilike.

ü  WAMARANGU:

Wanawake wa marangu ni wazuri sana wa umbo na sura ya kuvutia kuliko wachaga wengine wote. Lakini wanawachuna sana warombo, Wanawake wa marangu wana dharau sana na wanaume wa wa kimarangu ni waoga na washamba kuliko wanawake wao. Mwanamme wa kimarangu kupigwa na mke si jambo la ajabu maana wanadundwaga sana.

Ni utani tu wenzangu Wamarangu ila mbadilike. Ngaichoka kabsa na shindo icho.

ü  WAKIBOSHO:

Wanafanana sana na warombo kwa asilimia nyingi kuanzia unywaji wa pombe na mengineyo. Lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni kuchinja… wengi wao wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili sana… Mkibosho kukuchoma kisu sio jambo geni kwao na siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.  Usilete utani wala michezo na hawa watu maana kisu kitakukuta…. “nka kyandu”

Ni utani tu wenzangu Wakibosho ila mbadilike. Kukapa kyandu…kudosha kyandu…

ü  WAMACHAME:

Aisee hawa ni wezi sana ni watapeli mno, Ukifanya nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako makini sana kwenye maswala ya noti. Mmachame anaweza kukuua akiwa anatabasamu, sio waaminifu sana Ila ndio wachaga wanaoongoza kwa kwenda kanisani mara nyingi sana kuliko wenzao.

Wanawake wa kichaga huitwa “wapalestina” Inaaminika huwauwa waume zao wanapotajirika ili warithi mali. Wanawake hawa hawana umbo na sura ya kuvutia sana kama wachaga wengine, Wanapenda sana Uongozi wa kanisa na umaarufu kwa kujiita “Mangi” katika duka zao.

Ni utani tu wenzangu Wamachame ila mbadilike. Kutambashueny da ro wanawama’….

ü  WAURU:

Hawa hupenda kusoma lakini hawana maendeleo kabisa. Hadi leo eneo la “kishumundu” ni kama kiashiria cha wachaga washamba.  Wanawake wakifikia miaka 40 huwa wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni  wavivu lakini wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni yenye ndizi mbivu ukioa huru jiandae kulea…………

Ni utani tu wenzangu Wuruila mbadilike sasa.

ü  WASIHA:

Kwanza hawapendi kuitwa wachaga wanajiitaga watu wa west-kilimanjaro, Ni mchanganyiko wa wameru na wamasai. Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za ufundi na kilimo. Viazi vingi vya chips hutoka kwao, Wanawake zao wana vigimbi sababu ya kulima mno na kupanda panda vilima.

Ukitaka kuoa mkulima mzuri ambae ajapitia shule ila ni bora kuliko wa SUA nenda SIHA…

Ni utani tu wenzangu Wasiha ila mbadilike kidogo sasa.

ü  WAKIRUA:

Wanapenda sifa kama wahaya,  Wanawake wa kirua ni wachawi kupindukia… wanaloga hata  jiwe ili tu alikomoe. Wanaume wa kirua hawapendi kuoa kwao, Hawapendi kuishimjini wanaogopa gharama… lakini siku wakija mjini wawili utadhani wako mia maana sio kwa kelele hizo….

 

Ni utani tu wenzangu Wakirua  ila mbadilike.

ü  WA OLD-MOSHI:

Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda old-moshi inayoanzia moshi mjini. Maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saakumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.

Ni utani tu wenzangu Wa old-moshi ila mbadilike.

 

 

 MAWASILIANO


Tell+255 621 058168=whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com

Google: Mwalimu george boaz 

facebook: sirGeorge Boaz 

HAI

KILIMANJARO

 

 

Thursday, July 29, 2021

FONOLOJIA YA KICHAGA CHA KIMACHAME NA KISWAHILI.

 Fonolojia ya kimachame na kiswahili:

 
na mwandishi George Boaz swai na zabron



Kabila la wachaga ni kabila ambalo linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kabila hili hutumia lugha ya kichaga ambayo huwaunganisha wachaga wa maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo kama vile Machame, Kibosho, Rombo, Marangu, Siha, Kishumundu na Oldi Moshi. Kutokana na tofauti za kijiografia lugha ya hii imegawanyika katika vilugha (lahaja) ambapo vilugha hivyo hutajwa kimaeneo kama ilivyo hapo juu. Hivyo, katika ufafanuzi huu tutajikita katika kichaga cha MACHAME lakini tutatumia neno la jumla yaani kichaga. Kama ilivyo katika lugha ya kiswahili na lugha nyinginezo, lugha ya kichaga inaweza kuchanganuliwa katika vipengele mbalimbali kupitia tawi la isimu nyanjani kama ifuatavyo:

 

 1 Fonolojia ya lugha ya kichaga.

Kwa mujibu wa Roger (1994), fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia uamilifu, tabia na mpangilio wa sauti katika lugha. Kwa maana hiyo, fonolojia ni tawi la isimu linalojihusisha na uchunguzi, ufafanuzi na uchanganuzi wa sauti katika lugha mahususi kuanzia inapotamkwa, namna inavyotamkwa sehemu zinazohusika katika utamkaji na namna inavyosafiri na kupokelewa na msikilizaji. Dhana za msingi katika fonolojia ni fonimu na alofoni. Katika kipengele hiki tutaangazia fonimu za lugha ya kichaga kama ifuatavyo:

 

Fonimu

Sauti

Mfano

a

/a/

/amba/ - sema

b

/b/

/bara/ - pasua

c

/tꭍ/

/tꭍamԑtꭍa/ - pole

d

/d/

/dԑŋga/ - laani

e

/ԑ /

/ԑla/ - peta

f

/f /

/fɪꭍa/ - vunja

i

/ ɪ/

/ɪrɪꭍa/ - subiri

k

/k/

/kaꭍa/ - zamani

ky

/kj/

/kjaasɔ/ - methali

l

/l/

/ʊlaalʊ/ - sasa

Ly

/ly/

Lya - kula

n

/n/

/naa/ - kunywa

ng'

/ŋ/

/ŋana/ - kua

ny

/ɳ/

/ɳaɳ/ - mboga za majani

m

/m/

/mmɪ/ - mume

o

         /ɔ/

/ɔra/ - onyesha

p

/p/

/para/ - pasua

r

/r/

/raa/ - vaa

r

/ɣ/

/ɣa/ - acha

s

/s/

/sɔka/ - teremka

sh

/ꭍ/

/ꭍɪa/ - njia

t

/t/

/tԑɣԑβa/ - omba

u

/ʊ/

/ʊkwa/ - wehuka

v

/β/

/βandʊ/ - watu

w

/w/

/waa/ - uwa

y

/j/

/jԑwԑ/ - wewe

 

Katika uchambuzi huu, fonimu nyingi za lugha ya kichaga zinaendana na fonimu za lugha ya kiswahili lakini kwa baadhi ya fonimu kama vile /r/ na /v/ hutumika kulingana na muktadha wa matumizi. Katika baadhi ya maneno fonimu /r/ hutumika kurejelea sauti /r/ lakini katika maneno mengine huwakilisha sauti /ɣ/. Vile vile fonimu /v/ huwakilisha sauti /v/ na pengine hurejelea sauti /ß/.

 

2. Aina za maneno.

Aina za maneno ni mkusanyiko wa maneno yenye sifa zinazofanana ambayo huwekwa katika makundi mahususi. Mathalani maneno yanayotaja vitendo huwekwa katika kundi moja la vitenzi na maneno yanayotaja majina huwekwa katika kundi la nomino. Lugha ya kichaga ina aina mbalimbali za maneno lakini katika kipengele hiki tutaangazia aina nne ambazo ni Nomino, vitenzi, vivumishi pamoja na vibainishi kwa kutaja na kuonesha tafsiri zake katika Kiswahili. 

A. NOMINO.

Hili ni kundi la maneno ambalo hutaja majina ya watu, vitu, hali na mahali.

NA.

NOMINO ZA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

NA.

NOMINO ZA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

1

Ifua

Mfupa

 

21

Mbaka

Paka

2

Ifururu

Bundi

 

22

Mburu

Mbuzi

3

Ifuve

Nyani

 

23

Mmi

Mume

4

Ikite

Mbwa

 

24

Mmiku

Babu

5

Ikokoi

Panya

 

25

Mmbishwa

Shetani

6

Ikoru

Konokono

 

26

Mmbwa

Mvua

7

Ikunga

Samaki

 

27

Mwana

Mtoto

8

Iriso

Jicho

 

28

Mwi

Jua

9

Iruu

Ndizi

 

29

Saa

Nuru

10

Iruva

Mungu

 

30

Samu

Damu

11

Kana

Mdomo

 

31

Sava

Funza

12

Kasa

Pori

 

32

Soko

Maharage

13

Kiafuye

Kinyonga

 

33

Soori

Nguo

14

Kilwa

Chura

 

34

Shaa

Njaa

15

Kiri

Kiti

 

35

Shau

Dume

16

Kisaa

Makalio

 

36

Shoka

Nyoka

17

Kisangu

Uso

 

37

Shoonga

Chakula

18

Kishomba

Kiswahili

 

38

Shuki

Nyuki

19

Kisi

Kiuno

 

39

Ukari

Ugali

20

Kiriya

Nyundo

 

40

Uluko

Kijiko

41

Mai

Mama

 

46

Upata

Kata

42

Maruu

Ndizi

 

47

Uraato

Upepo

43

Urende

Mguu

 

48

Mangi

Mfalme

44

Usavi

Uchawi

 

49

Nlosha

Mwalimu

45

Uvayo

Unyayo

 

50

Nsongoru

Kiongozi

 

 

 

B. VITENZI

Vitenzi ni kundi lenye aina za maneno ambayo hueleza jambo lililofanyika, ambalo hufanyika, linalofanyika au litakalofanyika. Kwa ujumla hutaja matendo mbalimbali ambayo hufanywa kwa namna na nyakati tofauti. Miongoni mwa viitenzi katika lugha ya kichaga ni kama vifuatavyo:

 

NA.

VITENZI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

NA.

VITENZI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

1

Afua

Tambaa

 

11

Bara

Pasua

2

Akua

Kopa

 

12

Basha

Chonga

3

Amba

Sema/ pakaa

 

13

Dosha

Toboa

4

Ana

Lia/ shukuru

 

14

Ekyena

Hesabu

5

Anga

Ingia

 

15

Ekyera

Egesha

6

Angata

Futa

 

16

Ela

Peta

7

Ara

Laza

 

17

Faka

Kunya

8

Arannya

Sikiliza

 

18

Fina

Cheza

9

Ata

Washa/ ingiza

 

19

Fira

Kaba

10

Ava

Gawanya

 

20

Fisha

Vunja

 

 

NA.

VITENZI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

NA.

VITENZI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

21

Fumbuta

Ongeza

 

36

Kumba

Uza

22

Fwaaya

Samehe

 

37

Kummbwa

Kumbuka

23

Fweesa

Pooza

 

38

Kura

Kwangua

24

Illwa

Ng'oa

 

39

Lallwa

Bandua

25

Imuya

Pumzika

 

40

Lema

Kataa

26

Ira

Pita

 

41

Lelemba

Bembeleza

27

Irisha

Subiri

 

42

Lemba

Danganya

28

Isa

Chunga

 

43

Leta

Mimina

29

Ishura

Jaza

 

44

Lola

Angalia

30

Iva

Iba

 

45

Maa

Maliza

31

Kaba

Piga

 

46

Na

Kunywa

32

Kama

Kamua

 

47

Onga

Nyonya

33

Kira

Ponya

 

48

Raa

Vaa

34

Komba

Lamba

 

49

Tarama

Saidia

35

Kora

Pika

 

50

Ura

Nunua

 

Katika orodha hiyo, baadhi ya vitenzi vina maana zaidi ya moja mfano, "amba" ina maana ya kupakaa kama kupaka rangi lakini kwa upande mwingine ina maana ya sema kama kusema jambo. Hivyo muktadha wa matumizi na toni ndio hutambulisha maana iliyokusudiwa.

 

 

C. VIVUMISHI

Rubanza (2003:72-75) anasema kuwa kivumishi ni kipashio kitoacho habari zaidi kuhusu nomino. Kwa maana hiyo, tunaweza kusema kuwa hili ni kundi la maneno ambayo hufanya kazi ya kuifanya nomino au kiwakilishi kivume. Hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino au viwakilishi. Vivumishi vinavyopatikana katika lugha ya kichaga ni hivi vifuatavyo katika jedwali.

 

NA.

VIVUMISHI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

NA.

VIVUMISHI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

1

Shaa

Nyeupe

 

11

Shisha

Nzuri

2

Shaangu

Nyepesi

 

12

Shikasha

Mbaya

3

Shaasha

Ndefu

 

13

Siise

Embamba

4

Shiroo

Nzito

 

14

Shiwongye

Nene

5

Shuu

Nyeusi

 

15

Iilye

Safi

6

Shuumu

Ngumu

 

16

Ifani

Chafu

7

Rola

Tamu

 

17

Shidodoru

Nyekundu

8

Shifii

Fupi

 

18

Shikuu

Chakavu

9

Shiniini

Kubwa

 

19

Shiiya

Mpya

10

Shinnywa

Ndogo

 

20

Shinana

Laini

 

 

D. VIBAINISHI

Kibainishi ni neno ambalo hutumika pamoja na nomino nalo kwa kiasi fulani huweza kuonyesha ukomo wa maana ya nomino (Richards na Schmidt, 2002: 152). Vibainishi ni maneno ambayo hufanya kazi ya kutoa taarifa zaidi zinazoihusu nomino. Ni maneno yenye dhima ya kisarufi yanayotumika kuonyesha aina ya kirejelewa ambayo nomino hiyo inayo kama vile idadi, nafsi, uhusika, ngeli, dhamira na jinsi. Vipo vibainishi mbalimbali ambavyo vinapatikana katika lugha ya kichaga. Navyo ni:

 

NA.

VIBAINISHI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

 

NA.

VIBAINISHI VYA KICHAGA

TAFSIRI YAKE KWA KISWAHILI

1

Umwi

Mmoja

 

11

Ungi

Mwingine

2

Vavii

Wawili

 

12

Engi

Pengine

3

Vararu

Watatu

 

13

Toose

Zote

4

Vaana

Wanne

 

14

Tawo

Zao

5

Yeu

Huyu

 

15

Mfumbutu

Mwingi

6

Eva

Hawa

 

16

Shiingi

Nyingi

7

Valya

Wale

 

17

Fiingi

Vingi

8

Kulya

Kule

 

18

-eeru

- etu

9

Eyo

Hiyo

 

19

-afo

-ako

10

Yewo

Hao

 

20

-any

-enu

 

 

 

 

3. Ngeli za nomino.

Ngeli ni neno lililotokana na lugha ya kihaya "ingeli" lenye maana ya "kundi" au "aina". TUKI (1990) wanaeleza kuwa, ngeli ni kundi moja la majina yaliyo na upatanisho wa kisarufi unaofanana na viambishi vya umoja na wingi vinavyofanana. Kwa maana hiyo, ngeli inaweza kufasiliwa kuwa ni namna ya kuweka majina katika makundi yanayofanana au kuwiana kwa kuzingatia sifa za majina hayo. Uainishaji wa ngeli za nomino hufanyika kwa kuzingatia vigezo mbalimbali kama vile kigezo cha kutumia viambishi vya upatanisho wa kisarufi na kigezo cha umoja na wingi. Aidha katika uchanganuzi ufuatao wa ngeli za nomino za kichaga tutatumia kigezo cha upatanisho wa kisarufi pamoja na umoja na wingi.

 

 

 

NA.

NGELI

UFAFANUZI

MIFANO

1

 

A - VA

 

Hii ni ngeli inayojumuisha majina ya watu na nafasi zao. Majina kama vile Mwana (mtoto), Mwiisi (mchungaji), Mai (mama), Mfuru(daktari), Nde (baba), Nlosha (mwalimu) Mmiku (mzee), Nkyeku (bibi), Nsee (mtoto wa kiume)  na Nka (mke)

·         Mwana akelya

Vana vakelya

·         Mmiku ansha

Vamiku vansha

    

2

 

 

I - TI

Kundi hili huwa na majina ya wanyama, ndege na wadudu kama vile Ng'umbe (ng'ombe), mburu (mbuzi), nguve (nguruwe), fiko (fuko), nguku (kuku), saafu (siafu), sisiri (sisimizi), ngoru (mwewe),  shoka (nyoka), nre (nzige), mbaamba (kumbikumbi)

·         Mburu ikeana

Mburu tikeana

·         Nguku ikeshishwa.

Nguku tikeshishwa

 

3

 

KI - FI

Ngeli hii huwakilisha majina ambayo mwanzoni huwa na herufi KI. Majina hayo huweza kuwa ya vitu, wanyama na wadudu.  Majina hayo ni kama vile kiri (kiti), kyaandu (kisu), kibeni (kizibo), kimwi (kijinga), kilwa (chura), kifi (nyigu), kite (mbwa).

·         Kiri kikesongosywa

Firi Fikesongosywa

·         Kilwa Kikekillya

Filwa Fikekillya

4

LYI - A

Kundi hili huhusisha majina yote yanayoanza na kiambishi [i-] katika umoja na kiambishi [ma-] katika wingi mfano, iriso (jicho) - mariso  (macho), iyoo(jino) - mayoo (meno), isosoro(mjusi) - masosoro (mijusi),

Isembo(mjinga) - masembo(wajinga)

Irimbi(mshenzi)- marimbi(washenzi)

 

 

·         Iyoo elyi lyikevava

Mayoo yaa akevava

·         Iriso lyilolye fo

Mariso alolye fo

·         Isembo lyikeiya

Masembo akeiya

5

 

U

Hili ni kundi lenye majina ambayo huanza na kiambishi [u-] na ambayo hayana wingi. Mfano uraato(upepo), u

·          

 

 

A /KU

Hii ni ngeli inayoonesha mahali. Ni sawa na ngeli ya "PA/MU/KU" katika kiswahili. Katika lugha hii kuna viambishi viwili tu.

 

 

·         Ando alya aleera

·         Kundo kulya Kutanywe

·         Kulya kukeremwa

·         Yoo kuketirika

 

5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4. Mfumo wa uhesabishaji

Kama ilivyo katika lugha ya kiswahili na lugha nyingine, lugha ya kichaga ina namna ya uhesabuji wa namba kwa idadi zote zilizopo. Hii inadhihirika kama ifuatavyo.

i)Namba kuanzia moja hadi kumi.

o   Kimwi - moja

o   Fivii - mbili

o   Firaru - tatu

o   Fiina - nne

o   Firanu - tano

o   Firindaru - sita

o   Mfungare - saba

o   Nyanya - nane

o   Kyenda - tisa

o   Ikumi - kumi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

i) Makumi, kuanzia kumi hadi mia moja kwa kigawe cha kumi kwa mumi.

o   Ikimi - kumi

o   Makumi avii - ishirini

o   Makumi araru - thelathini

o   Makumi aana - arobaini

o   Makumi aranu - hamsini

o   Makumi arindaru - sitini

o   Makumi mfungare - sabini

o   Makumi nyanya - themanini

o   Makumi kyeenda - tisini

o   Iyana - mia moja

 

iii) Mamia, kuanzia mia moja hadi elfu moja kwa kigawe cha mia kwa mia.

o   Iyana - mia moja

o   Mayana avii - mia mbili

o   Mayana araru - mia tatu

o   Mayana aana - mia nne

o   Mayana aranu - mia tano

o   Mayana arindaru - mia sita

o   Mayana mfungare - mia saba

o   Mayana nyanya - mia nane

o   Mayana kyenda - mia tisa

o   Kyiku - elfu moja.

 

Mfumo huu wa uhesabishaji unazingatia mfumo wa hesabu wa mamoja, makumi, mamia, maelfu na kuendelea. Baada ya kutaja namba kubwa ndipo namba nyingine hufuata kwa kadiri ya udogo wake kama ilivyo katika lugha ya kiswahili. Mfano, "Kyiku kimwi na mayana avii na ikumi"  yaani elfu moja na mia mbili na kumi. Pia baada ya kila kundi moja la namba (1-9) uhesabuji hufanywa kwa kurudia au kuongeza namba za awali. Mfano baada ya kufika kumi, ili kuendelea unarudia tena kuitaja kumi na kuongeza namba za mwanzoni yaani moja hadi tisa ndipo ufike katika kundi lingine. " ikumi + kimwi = ikumi na kimwi, mayana avii + kimwi = mayana avii na kimwi".

 

5. Mfumo wa uitaji majina kwa watu.

Mfumo wa uitaji majina hutofautiana baina ya jamii na jamii. Katika kabila la wachaga watu hupewa majina kama sehemu ya kuwatambulisha kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo ni pamoja na hali, ukoo, dini pamoja na idadi ya wazaliwa. Hivyo, tutaanza kufafanua kipekngele kimoja baada ya kingine kama ifuatavyo:

a) Hali

Hii inahusisha hali inayokuwapo wakati mtoto anazaliwa hivyo kupelekea kuitwa jina linaloendana na hali hiyo. Majina hayo ni pamoja na:-

·         Ifura - Furaha (hutokana na hali ya furaha)

·         Nsia - Tumaini (hutokana na hali ya kupata tumaini baada ya masumbuko)

·         Ndetyefyose - Baba ameyasikia yote ( hutokana na hali ya kupata tumaini)

·         Alewarywa - Aliyepokelewa (Ni jina la mtoto aliyesubiriwa kwa shauku kubwa)

·         Widimi - Uwezo (ni jina linaoonyesha hali ya kuwa na uwezo wa kupata watoto)

 

b) Idadi ya wazaliwa

Kila mzaliwa katika familia huwa na jina lake la jumla. Majina haya huwataja babu na bibi wa pande zote na hulenga kuonyesha heshima pamoja na kuendeleza undugu na mshikamano wa familia na ukoo kwa ujumla. Aidha jina la mtoto wa kwanza ni moja kwa kila mtoto wa kwanza kwa kuzingatia jinsia. Majina haya si mahususi yaani siyo ya mtu binafsi ( jina la shule au ubatizo) bali ni ya nyumbani. Majina hayo ni kama yafuatayo.

·         Mkuu/ Meku/ Nkuu-  Jina la mzaliwa wa kwanza wa kiume. Humtaja babu kwa upande wa baba kwa maana hiyo "nkuu/ Meku" ni vifupisho vya neno "mmiku" yaani babu.

·         Kyekuwe - Hili ni jina la mzaliwa wa kwanza wa kike. Sifa zake ni sawa na zinazorejelewa na zile za mzaliwa wa kwanza wa kiume lakini humrejelea bibi. Ni jina lililotokana na neno "nkyeku" likiwa na maana ya bibi na kiambishi "we" humaanisha "yake" hivyo ni sawa na kusema bibi yake. Hii ni kwa upande wa baba.

·         Ndeyanka - Ni jina la mzaliwa wa pili wa kiume. Jina hili humtaja baba mzaa mama (baba mkwe). Katika jina hili neno "nde" humaanisha baba halikadhalika neno "nka" humaanisha mke na "ya" ni kiunganishi. Kwa maana hiyo ni sawa na kusema baba wa mke yaani baba mkwe.

·         Mayeanka/ Manka - Hili ni jina la mzaliwa wa pili wa kike. Ni jina ambalo humtaja mama mkwe au bibi kwa upande wa mama ambapo "ma/maye" ni mama, "a/ya" ni viunganishi na "nka" ni mke. Hiyo, ni sawa na kusema mama wa mke yaani mama mkwe.

·         Mamii - Ni jina la mzaliwa wa tatu wa kike. Humtaja mama mzaa baba yaani babu kwa upande wa baba. Limetokana na maneno "ma" ikiwa ni kifupisho cha "maye a" "yaani mama wa" pamoja na neno "mii" likiwa na maana ya "mume". Hivyo hutaja mama wa mume ambapo ni sawa na mama mzaa baba.

·         Ndammi - Hili ni jina la mtoto wa kiume linalomrejelea babu kwa upande wa baba. Hili huweza kuwa kwa mzaliwa wa tatu na kuendelea japo ni sawa na jina la mzaliwa wa kwanza.

Katika orodha ya wazawa wa kiume kuanzia wa tatu na kuendelea jina la " Nkuu" huendelea kwa kurejelea babu kwa upande wa baba. Hutajwa kwa hesabu kuanzia wa pili hadi wa mwisho kulingana na idadi iliyopo yaani, "nkuu wa kavii (wa pili)",  "wa kararu (wa tatu)" na kuendelea. Mathalani kwa wazawa wa kike "Mamii" pia huendelea kwa kumtaja bibi kwa upande wa baba kama ilivyo kwa upande wa wazawa wa kiume.

 

c). Dini ( Kikristo)

Baada ya ujio wa wamishenari katika eneo la uchagani watu waliopokea mafundisho walibatizwa na kuwa wafuasi wa dini ya kikristo. Hii ilipelekea kuiingiza dini katika mfumo wa lugha ili kuweza kuendeleza shughuli za kidini. Vitabu vya dini hususani Biblia vilitafsiriwa kwa lugha ya kichaga yakiwemo majina ya waandishi na watu waliotajwa katika vitabu hivyo. Hivyo watu hupewa majina mara baada ya kubatizwa. Majina hayo ni pamoja na haya yafuatayo:

·         Anandumi - Mshukuru Bwana

·         Anande - Mshukuru Baba (Mungu)

·         Eliakunda - Mungu amependa

·         Elianshisauwa - Mungu amenichagua

·         Elianshiwinya - Mungu amenishindia

·         Rumishaeli - Mtukuze Mungu

·         Aranyandumi - Msikilize Bwana

·         Ndemfoo - Baba (Mungu) ni mpole

·         Shikusiriyaeli - Ninamtumaini Mungu.

·         Simboyande - Kipawa cha baba (Mungu)

 

d) Koo (ukoo)

Ukoo ni muunganiko wa familia zenye asili moja. Ni vizazi mbalimbali vilivyotokana na familia moja. Majina ya ukoo hutambulisha watu kuwa wametokea katika familia fulani. Aidha kila mtoto anayezaliwa katika familia ya ukoo fulani hupewa jina la mwisho la ukoo wa familia hiyo. Hata mwanamke anapoolewa pia huwa na jina la ukoo wa familia ambayo ameolewa. Miongoni mwa majina hayo ni haya yafuatayo:

·         Swai

·         Sawe

·         Kimaro

·         Lema

·         Mushi

·         Nkya

·         Urassa

·         Usiri

·         Ulomi

·         Mmbasha

6. Lugha na jinsia

Katika lugha ya kichaga, lugha hutumiwa kulingana na jisia katika baadhi ya shughuli mbalimbali za kila siku. Kuna maneno ambayo huwakilisha jinsia moja tu na mengine huwakilisha jinsia zote. Kwa msingi huo lugha hujipambanua katika vipengele vifuatavyo:

a) Salamu

Kuna salamu ambazo hulenga jinsia ya kike tu na zile ambazo hulenga jinsia ya kiume. Salamu kwa upande wa jinsia ya kike huwa na neno "ma" kumaanisha mama, "kye" kumaanisha binti au msichana na "nkwe" kwa maana ya mtu yeyote wa kike. Mfano,

·         Neantwa ma - salamu ya asubuhi kwa mama

·         Nesindiswa kye - salamu ya mchana kwa msichana au binti

·         Kwalollya nkwe - salamu ya jioni kwa wanawake wote

Kwa upande wa jinsia ya kiume, salamu huwa ni ile ile lakini huwa na maneno ambayo hurejelea jinsia ya kiume mwishoni. Neno "mbe" huwakilisha mtu ambaye ni baba, "mae" huwakilisha kijana wa kiume na "nsee" huwakilisha kijana mdogo. Aidha wakati mwingine "mbe" hurejelea wanaume wote. Mfano,

·         Neantwa mbe - Salamu ya asubuhi kwa mtu mzima (baba).

·         Nesindiswa mae - Salamu ya mchana kwa kijana.

·         Kwalollya nsee - Salamu ya jioni kwa mtoto. ( pia hutolewa baada ya kazi)

 

b) Majina

Utoaji wa majina huzingatia jinsia. Kuna majina ambayo ni ya wanawake na mengine ambayo ni ya wanaume tu. Majina hayo ni pamoja na yale ya idadi ya wazaliwa. Mfano:

Wanawake.

·         Manka

·         Kyekuwe

·         Mankya

·         Mansabu

·         Mamii

Wanaume

·         Ndeyanka

·         Babuu

·         Meku

·         Nkuu

·         Ndeanshau

 

 

 

Kwa ujumla, Lugha ya kichaga ni lugha inayojitosheleza kwa kuweza kukidhi haja ya mawasiliano katika shughuli mbali mbali. Aidha hutumika katika maeneo ya nyumbani, katika vikao vya vijiji pamoja na kanisani. Lugha hii pia ina maandiko mbalimbali ikiwemo vitabu vilivyotafsiriwa kutoka lugha nyingine. Miongoni mwake ni kitabu cha Agano jipya, Biblia pamoja na vitabu vya nyimbo za ibada. Kwa maana hiyo, ina uwezo wa kuchanganuliwa kupitia taaluma ya isimu kama ilivyo katika lugha ya kiswahili.

 

 MAREJELEO

Lass, R. (1984). Phonology: An introduction to Basic Concepts. Cambridge: Cambridge Textbooks in Linguistics.

Richards, J. C & Schmidt, R. (2002). Longman Dictionary of Language Teaching and Applied Linguistics: 3rd Edition, London: Pearson Education Limited.

Rubanza, Y.I (2003). Sarufi: Mtazamo wa Kimuundo. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

TUKI (1990). Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar  es Salaam: TUKI.


Kwa maoni ushauri nitafute kwa:


MAWASILIANO

Tell+255 621 058168=whattsapp

sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com

Google: Mwalimu george boaz 

facebook: sirGeorge Boaz 

HAI

KILIMANJARO