Kinukamori water falls ni sehemu ya maporomoko ya maji yenye urefu mkubwa sana ambayo inapatikana katika mkoa wa KILIMANJARO marangu Tanzania, Ni umbali wa dakika 45 kutoka barabara kubwa ya dar>arusha au (himo). Licha ya kuwa na maporomoko makuwa yenye kustaajabisha kila afikae apo. Huwa pia na kijani kibichi na aina mbalimbali za ndege wanaotoa sauti nzuri zenye naksi na milio mizuri usikiapo masikioni mwako. huwa na viumbe wengine kama vile vinyonga mapango na vingine vingi.
Mbali na apo utapata historia ya kusisimua kuhusu binti MAKINUKA.
Makinuka alikuwa ni binti wa kichaga(marangu) ambaye zamani alipata ujauzito kabla ya ndoa(mimba za utotoni). Alilazimika kufukuzwa nyumbani kwa wazazi wao kwani mila na desturi za kichaga(marangu) hazikuhuruhu binti kuzalia nyumbani au kupata mimba kabla ya ndoa, na mngefanya hivyo mngepewa adhabu kali wote wawili yaani msichana na mvulana waliohusika walitakiwa kuuliwa.
Makinuka kutokana na kufukuzwa nyumbani kwa sababu ya kupata mimba kabla ya ndoa aliamua kwenda katika maporomoko ya kinukamori kujitosa ili kukwepa kuuliwa pamoja na mpenzi wake(mkaka aliyempa mimba) alitaka afe yeye tu.
Wakati alipofika katika maporomoko hayo ya maji kutaka kujirusha ili afe, Aliona si vyema kujiua pamoja na kiumbe asiye na hatia(mimba) wakati huo mama yake alikuwa nyumba kumshawishi kuwa asifanye hivyo.
Aliamua kurudi ili kuja nyumbani kuwaomba wazazi wake msamaha kwa kosa alilolifanya.
Lakini alipogeuka kuanza kurudi nyumbani ili kuja kwa wazazi kuwaomba msamaha kwa kosa alilofanya. ghafla alimwona CHUI akimnyatia kwa lengo la kumkamata amle, Akaona hana namna ya kumkwepa chui huyo alijikuta ameelekea kule kwenye maporomoko yale marefu alijirusha katika maporomoko hayo na kufariki dunia. Na huo ndio ukawa mwisho wa msichana MAKINUKA.
Kwa mila na desturi za kichaga kwa wakati wa miaka ya nyuma mtoto wa kike akipata mimba kabla ya kuolewa (mimba nje ya ndoa) adhabu kali ilitolewa kwa wote. mwenye mimba na aliyempa mimba, Adhabu yao ilikuwa ni kulaliana mmoja juu na mwingine chini halafu wanachomwa mti mgongoni ambao unawachoma wote hadi wafe..
Kwa maoni ushauri nitafute kwa:
MAWASILIANO
Tell+255 621 058168=Whattsapp
sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com
Google: Mwalimu george boaz
facebook: sirGeorge Boaz
intagramu officialsirgeorge
HAI
KILIMANJARO
Safi sana
ReplyDelete