Thursday, February 6, 2020

VYAKULA VYA KICHAGA 10 NA UPIKAJI WAKE.


KARIBU.. natanguliza shukrani zangu za dhati kwa MUNGU kwa kunijalia afya na uzima.pili ni kwako mdau wa blogger yangu ya kuhifadhi mila na kuendeza utamaduni wa kichanga MUNGU AWABARIKI..

CHAKULA.. ni moja ya viashiria vya kabila(element of culture) yaani utambulisho wa kabila mfano: WASUKUMA hupenda ugali WAPARE samaki WACHAGA ni ndizi.. hivi ndo vyakula vikuu kwa kabila hizi.

LEO NAPENDA KUKULETEA VYAKULA VYA KICHAGA NA UPIKAJI WAKE.



1.NGARARUMU
mahitaji. mahindi makavu,maharage,chungu maji magadi kuni mwiko (chumvi ukipenda)
HATUA ZA UPISHI.
washa moto injika chungu jikoni kikiwa na maji weka mahindi(yaliyochambuliwa) weka magadi chochea moto hadi yaive EPUA. osha mahindi hayo mara mbili kwa maji safi injika chungu tena jikoni kikiwa na maji na maharage kisha weka mahindi (uliyoyapika
na kuosha)juu ya maharage weka magadi/chumvi CHOCHEA TENA HADI YAIVE kikiiva epua weka kwenye ngata(kitako cha chungu) kisha chukua mwiko songa UKIMALIZA Ni tayari kwa kula 
NB:huwa kizuri ukila kwa chai au maziwa.
magadi; Hulowanishwa kwanza kwenye maji.


2.MALAA
mahitaji... ndizi laini/ng'ombe au mtori maziwa mgando chungu upekecho 
HATUA ZA UPISHI
washa moto injika chungu chenye maji weka ndizi uliyochagua mfano ndizi mtori(ziwe zimemenywa zimekatwa vipande vidogo kiasi)CHOCHEA  kikiiva EPUA chungu PEKECHA NDIZI HIZO weka maziwa pekecha
UKIMALIZA NI TAYARI KWA KULA
NB:chakula hichi hakiwekwi magadi


3.NYANYI
mahitaji....Ndizi ng'ombe/mtori mnavu/kimashigha/sosoko majani ya kunde maziwa mgando maji chungu upekecho nk
HATUA ZA UPISHI HUU
Washa moto injika chungu chenye maji  weka ndizi (zimemenywa na kukakwa vipande vidogo vidogo) CHOCHEA ZICHEMKE tia mboga mfano mnavu(zioshwe na kukatwa) ACHA ZIIVE PIA. zikiiva epua PEKECHA weka maziwa pekecha pia.. UKIMALIZA NI TAYARI KWA KULA.


4.MISHARE YA MMBALA.
Mahitaji.. Ndizi mshare magadi chumvi maji chungu.
HATUA ZA UPISHI HUU.. Washa moto injika chungu jikoni chenye maji na magadi (chumvi sio lazima ila weka  kama unapenda) weka ndizi zilizomenywa(usizikate/usizipasue)CHOCHEA HADI ZIIVE. zikiiva epua jikoni PAKUA NI TAYARI KWA KULA

5.KIMANTINI.
mahitaji. ndizi mshare maji chungu upekecho magadi chumvi
HATUA ZA UPISHI HUU
Washa moto injika chungu jikoni weka  ndizi (ziwe zimeoshwa walau mara mbili kwa maji safi ZIKATWE VIPANDE VIDOGO VIDOGO) weka maji na magadi CHOCHEA  kikiiva unapekecha  UKIMALIZA NI TAYARI KWA KULA 
NB: NI KAMA KIBURU SEMA HAKINA MAHARAGE TU.
6. KIBURU.
 Mahitaji na upishi wake hautofautiani sana na upishi hapo juu.
HATUA ZA UPISHI HUU.
Washa moto injika chungu chenye maji weka maharage kisha ndizi (zikatwe vipande vidogo vidogo zioshe walau mara mbili kwa maji safi na salama) CHOCHEA weka magadi (chumvi kama unapenda) CHOCHEA TENA KIKIIVA EPUA. pekecha ukimaliza ni tayari kwa kula.


7.MTORI.
hichi ndo chakula kimachopendwa sana na wachaga wengi.
mahitaji... Ndizi mtori/ng'ombe chumvi karoti hoho sowe viazi mbatata kitunguu mafuta upekecho maji chungu
 MAPISHI YAKE.. kutokana na chakula hichi kupendwa kimekuwa na upishi tofauti tofauti
HATUA ZA UPISHI
washa moto injika chungu chenye maji weka nyama(iliyooshwa na kukatwa vipande vidogo vidogo) chemsha weka chumvi ikiiva punguza supu  kidogo weka ndizi sowe viazi mviringo (hoho karoti kitunguu na mafuta kama wapenda) chochea kikiiva SONGA/PEKECHA weka supu kukifamya kuwa laini UKIMALIZA epua ni tayari kwa kula 
NB:wachagga hupendelea kula sana chakula hichi jioni/usik u

contract 0621058168 whattsapp

3 comments:

061058168