MAWASILIANO

SURA YA PILI 

MAWASILIANO

Mawasiliano: Ni kitendo cha kupashana habari,kubadilishana maarifa na ujuzi.

AINA ZA MAWASILIANO

Mawasiliano ya zamani(utamaduni) hutumia njia za asili kupashana habari au kubadilishana maarifa. Mfano wa aina hii ni filimbi,ngoma na baragumu.Hutumika sana vijijini kwa karne hii ya 21. Ukisikia baragumu linalia huashiria jambo fulani kutokana na mlio unaosikika . Mfano huweza kuashiria kutoa taarifa nzuri au mbaya.

Mawasiliano ya kisasa: kutokana  na utandawazi pamoja na mwingiliano wa jamii na mataifa. Mawasiliano ya asili yaliadhiriwa kutokana na jamii kuacha njia zao za asili za kupashana habari hivyo basi mawasiliano ya kisasa yakachukua nafasi kubwa katika karne hii ya 21 kutokana kuwa na urahisi , uokoaji wa muda pia kuonekana nzuri na kisasa zaidi.

NJIA ZA MAWASILIANO

1: Mawasiliano kwa njia ya maandishi au matamshi

2:Mawasiliano kwa njia ya ishara

3: mawasiliano kwa njia ya alama

Mawasiliano kwa njia ya maandishi: Mawasiliano ya njia hii hutumia matamshi au maandishi . Mfano barua na mazungumzo.

Mawasiliano kwa njia ya ishara: Mawasiliano haya hutumiwa na watu wenye lengo la kupashana habari wenyewe kwa wenyewe. Mfano (vikosi vya jeshi) na madereva. Pia mawasiliano haya hutumiwa na watu wenye ulemavu wa kusikia(viziwi) kama njia ya mawasiliano kwa kutumia ishara katika viganja vya mikono yao pia miondoko ya miili yao (mwanzo 9:13).

Mawasiliano kwa njia ya alama: Mawasiliano haya hutumiwa na watu mbalimbali,kwa lengo la kuelekeza,kuonya  na kutoa tahadhari kuhusu vitu au vifaa mbalimbali  hususani kwa madereva,marubani, naodha na wanasayansi .

Najua utajiuliza kwa nini nimekueleza haya pengine umewaza nimekurudisha darasani au laaa !!. Bali napenda uongeze ufahamu tuu juu ya  mada ya mawasiliano . Pia kwa kufahamu mada hii ya mawasiliano itakusaidia kujua njia ipi sahihi katika kuwasliana na MUNGU pia mwanadamu mwenzio . MUNGU anaweza kutumia njia kati ya hizo hapo juu katika kukuonya, kukufundisha au kutumia karama yako .

ushawahi kujiuliza juu ya maajabu ya MUNGU kuhusu mawasiliano ?

NJIA ZINAZOWEZA KUKWAMISHA MAWASILIANO

Kuna vyanzo vingi vinavyoweza kusababisha kukwama kwa ujumbe au taarifa kumfikia mlengwa kama ilivyokusudiwa . Baadhi ya vyanzo hivyo ni:

Kutumia njia isiyo sahihi . Kwakutokuchagua njia sahihi ya mawasiliano ujumbe wako waweza kukwama. Mfano kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa kusikia usipo tumia mawasiliano  kwa njia ya ishara ujumbe wako hautamfikia.

Lugha. Katika nchi yetu  kuna makabila 120 na kila kabila huwa na lugha rasmi ya kuwasiliana (lugha mama) mtu wa kabila moja akihitaji kuwasiliana na mtu wa kabila lingine hutumia lugha ya taifa(Kiswahili).Iwapo hawatatumia lugha ya taifa na kutumia lugha mama mawasiliano hukwama kwani lugha hizo zimetofautiana kimatamshi na kimaana pia . Epuka kutumia lugha zaidi ya moja katika mawasiliano yaweza kuleta kutokuelewana. (mwanzo 11:7).

Mandhari. Unaposhindwa kuendana na mandhari ujumbe au taarifa huweza kukwama. Mfano unapokuwa msibani, unatoa ujumbe wa  kuchekesha, huweza kutafsiriwa vibaya kwa kuwa watu wapo katika majonzi. Wapaswa kutumia ujumbe wa faraja.

Ushawahi tumia muda mrefu kufikisha ujumbe? Nini kilipelekea ? ulitatuaje?

FAIDA ZA MAWASILIANO

Kuimarisha uhusino/mahusino

Kukuza ujuzi na stadi za maisha

Kujipatia ajira

Kukuza uchumi

Kufikisha ujumbe au taarifa kwa walengwa 

Unadhani mawasiliano yana faida kwako? Ungekuwaje ungekosa mawasiliano?


No comments:

Post a Comment

061058168