MISEMO YA KICHAGA 100 (machame) NA MAANA YAKE Fyaaso makumii iyana fya kimashami.
maneno ya kichaga cha machame na maana yake.
Kwanza natanguliza shukrani zangu kwa Mzee Boaz swai na Bi Josephine swai pamoja na mdogo wangu mpendwa Celina Boaz (mziwanda) kwa kunipa ushirikiano katika suala hili la kuandaa makala hii nzuri ya kimachame.
1.Muna shoonga=Mtoto ni chakula.
2.Kite maae= Mbwa ni mama yake.
3.mwaafu mmbeiye nyama shiwanri immaye ukuwi=mlafi mkatie nyama nono imkinaishe.
4.Amba ukiva n'lwakwa, kulaambe nlweru-fo= sema shida ni yangu usiseme ni yetu.
5.Irwa-rwa ni ndoo na ikaa mau= mtembea bure si sawa na mkaa bure/kutembea ni kujifunza mengi.
6.Kirendeeya kiishi mangi-fo= ajali haimjuhi mfalme
7.Kulaalwe ukwe waaro-fo=Tusing'anga'anie vya kuomba.
8.Kulakushele na nlota wa nsoro ungi-fo= usisafirie nyota ya mwenzako.
9.Kwakumbwa ya makambo nkulala rwe-fo=yaliyopita si ndwele.
10.Kwalemba nrini nkwi kurwaa nafo mwanao?= Usimtukane ngariba uzazi ungalipo/usimtukane mamba kabla ya kuvuka mto.
11.Kwalala kufii na mangi nkukumbwa irunda-fo=Ashibae kila siku hatakumbuka kufanya kazi.
12.Kishapu kya kana mmbo kiraa ngota kya iirupa=mdomo hutoa maneno matusi ya kuchefua kuliko ushuzi.
13.Ndumi akapoo ifumu limwi-fo=mwanaume auliwi na mkuki mmoja.
14.Uroko ngatara= uvivu ni umaskini.
15.Mangi mbandu=Uongozi/ufalme ni watu.
16.Ando mangi akai nkurumbukau ndeye-fo=penye utawala bora sheria hufuatwa.
17.Kinungu kitula mmbo kyelema irika
18.Kilwa kikaamba shiwikaa mwana wakwa nsee, Na ukyele lukairikya neeny-da= chura akisema ntamvika mtoto wangu mkufu, Mtoto wake huruka mbali kuliko.
19.Ing'uruu llyitura mammi-fo= chongo hakosi mwenza.
20.Fira shiikimbe nnyilyee ng'aumbe-fo= Tahadhali ni kinga ya balaa.
21.Fyandu fivii nfikaa kibony kimwi-fo=mafahali wawili hawakai zizi moja.
22.Eeshi aviyoo=Anajua aambiwacho.
23.Ando mburu ilelyiya mmbala nnyenda-u lyimwi-fo= Pende uhondo hapakosi hodi hodi kila saa.
24.Ifuwe llyilolyaa numa ya wayo-fo= nyani haoni kundule
25.Ando kulashuuta-u weesi utau ndeu=Sehemu usioweza kutoa kikubwa toa apo kidogo.
26.Ikarang'a llyaara na mwana keenda=malezi ni utotoni.
27.Iwo lya nsoro ni ifirya ndi=kuanguka kwa mwanaume ni kupiga magoti/kusalimu amri.
28.Kookya meengi maata mmbo ashoongwaa=mtaka yote kwa pupa hukosa yote.
29.kookya ukiva au utondo lluyaa-fo= shida haina kwao.
30.Kwafigya nre nkusheny mmbo tirafunaa nkusha=chelewa chelewa utakuta mtoto si wako/Bandu bandu humaliza gogo.
31.Kwiikundye iilwa isya ilwa mbele ngerengere=ukitaka kufanikiwa katika maisha ondoa kwanza vikwazo.
32.Lema ura lwiikee ushu=samaki mkunje angali mbichi.
33.Kya nkunde kiporaa iru=Wema hauozi.
34.Kwalya na mangi kulankumbe kana-fo=Ukishiba na mkubwa usiseme siri zake.
35.Fiko ikalema kitei nnyilema kitambasii-fo=Fuko akishindwa mtego awezi kutataa uzi wa kutega.
36.Uninii shumbi/mmbala=ukubwa ni dawa.
37.Fira eende wafo=Vitani ni kukutana na wakwako.
38.Esa ruwa nsengye=fikiri kabla ya kutenda.
39.Ando kooka nndu mmbo ariirwa-u ndu=Panapotoka kitu hurudisha kitu.
40.Kilwa nkiseswaa nkya-fo=chura haiulizwi mkia.
41.Kimburu kya tora ntambatamba= Debe tupo hulia.
42.Kwatia iriti muro mmbo lyikumaraa=shukrani ya punda ni mateke.
43.Kwasikya ufu nkusikyaa kyiyio-fo- mficha maradhi kifo humumbua.
44.Ing'ana n'yirambuka=kukua ni kupambanua.
45.Kulaarafume kulaore ifua lyammaanga wookony-fo= usishukuru kabla ya kupewa.
46.Kiteende mmbo kivee ndu=Maskini huweza kuamka tajiri.
47.Nree ngama=Kazi ni asubuhi.
48.Kwakapa mmbwa na iriso mmbo lyishiyaa=Ukiumiza pua na sikio hulia.
49.Vandu masaa=watu ni mali.
50.Ikunda llyipwaa-fo=wema hauozi.
51.Kisumu kya mamwiingi nkiviraa ikundu-f0=Penye wengi kuna mengi.
52.Kwanlwaa mmbo kukee kipule kya waanga=Ukiugua ndio kula ya mganga.
53.Iwia mmbo lyefuma nunguny lyikawo rukony=mruka mkojo hukanyaga kinyesi.
54.Kyooka nrweny kikawooya okony=Kimetoka kwake kikarudi kwake.
55.Ikooru lyikaamba, kweenda waaiyo mmbo kukiiya fongo ta ndu ivii= mtembea pole hajikwai.
56.Kya nkunde kiporaa iru=pendo kwa uumpendae haliozi.
57.Kyimwi kyo kiwoonisa ikumi= moja ndio huzaa kumi.
58.Kiwaka nkirekaa-fo Asili haipotei.
59.Mushu nnyirekaa-fo=mila haipotei.
60.Kite nkikuuyaa waasiony-fo=Mtu ni kwao/mdharau kwao ni mtumwa.
61.Kite kikammiluka mayoo nkikiidimaa imara-fo=Mbwa mzee hawezi kungata.
62.Kite kikammiluka mayoo nkikiidimaa iringa poo-fo=mbwa mzee hawezi kulinda nyumbani.
63.ngukuu ifufulaa nyo iwura=kuku anayechakura ndio anaye shiba.
64.Kifurumba au kififi mmbo kyeema nndu iraiya muu=Wivu ndio huponza kutokuendelea.
65.Samu nshiroo ngota mura=Damu nzito kuliko maji.
66.Isoka lyiishi munyi=mtu hujua wake.
67.Ishaaswaa isikyoo iriso=funika kombe mwanaharamu apite.
68.Ikisinda n'reminy mmbo yasia muye=subira yavuta heri.
69.Kwelolya nremi wa mbai wiilyiwaa na numa mmbo ulatyaa wafo=mwenzako akinyolewa zako tia maji.
70.kwitanaa mmba wika-fo ngwe ta ndiiri=Ukiwa unajenga weka huko nguzo imara.
71.Urokoo ngatara=uvivu ni umaskini.
72.Uniiny nyi nrii=ukubwa dawa.
73.Akee kufii na irambaa nyawoiwa nalyo-fo=aliyeko karibu na mti aangukiwi nao.
74.Nkushaa/mbushaa mbumasana-fo=biashara haigombi.
75.Ikasana seelyo ifika-fo=kukazana sio kufika.
76.Arungutaa nrwee nyalala shaa-fo=Ajishughulishae alali njaa.
77.Kwalolya vana wa miiso na maaye nnyoo kufii akai=Ukikuta watoto wa chui, mama yao yupo apo karibu.
78.Kuleele wakongingo-fo=Usidharau asiyekuwa nacho.
79.Kiteende mmbo kivee nndu=
80.Kite kilandewio baada nkyandemaara-fo=Mbwa hung'ata baada ya kusaksiwa.
81.Kookya meengi maata mmbo ashoongwaa=Mla vingi huvimbiwa.
82.Kinungu kitula mmbo kyelema irika=mbaya hutengwa na jamii.
83.Nshele mbaana=Furaha ni watoto.
84.Mbuya nyi-nri=Rafiki ni dawa.
85.Lyafo ni lyafo na lyikasukya ao lyikananyaa=Mtu ni ndugu yake hata kama ni kilema.
86.Kweenda na kite waasieny nkiwuyaa fo= Ukienda na mbwa machinjioni hakitarudi.
87.Kwaantya muro irininy mmbo udukyaa=Mzua janga humfika.
88.suwana ntilee ando amwi-fo= Mafahali mawili hayakai zizi moja.
89.kuleere iwe ruweny ikusyedo-fo=Usimchokozi mkimya.
90.Koota kite irinin mmbo kikumaraa=shukrani ya punda mateke.
91.koota ngashe mmbo ikukapaa inanga= Ukiwa unamtoa ndama atakupiga teke.
92.Kana ntitiraa muni fo= uongo hauna muhusika.
93.Kinungu kitula mmbo kyekema irika=mwovu hutengwa na jamii.
94.Nungu ibarikya mwoongony=chungu hupasukia mlangoni.
95.Mfe umwi mmbukora mmba=Njiti moja huchoma nyumba.
96.Kindo kyeema kikwa kisheeta ni iwe kwasii ya wayo= maendeleo hukwamishwa na vikwazo.
97.Kulasaamise mfongo ando ulasaama-fo= Usilazimishe maji kupanda mlima.
98.Nrema sinde ya mfongo= Lima kando ya mfereji.
99.Kweeta mwana eshiyiaa nnyakenkape-fo=Ukiona mtu analalamikia maafa maafa, Jua Maafa hayajampata.
100.Kweeta kapa, kulaambe waa-fo Amba tira shishe, Kulakooye ansandyo-fo wafo= Ukiskia piga, Usiseme ua maana unaweza kuta ni mtu wako.
Shukrani zangu za dhati ni kwako wewe mdau wangu wa nguvu wa tovuti hii.
Natumaini umefurahi sana kwa kufahamu misemo ya kichaga.
Kwa maoni ushauri nitafute kwa:
MAWASILIANO
Tell+255 621 058168=whattsapp
sirgeorgeboazndeyanka09@gmail.com
Google: Mwalimu george boaz
facebook: sirGeorge Boaz
HAI
KILIMANJARO